720 B
720 B
Maelezo ya jumla
Katika mistari ya 1-18, Nebukadneza anaeleza maono yake kutoka kwa Mungu katika nafsi ya kwanza
Ni uamuzi uliofanya na yeye aliye mtakatifu
Kauli hii yaweza kuelezwa katika muundo tendaji. "Yeye aliye mtakatifu amefanya uamuzi."
mtakatifu
Kirai hiki huenda kinawarejelea Malaika. "Malaika watakatifu"
hao walio hai
"kila mtu aliye hai" au "kila mtu"
huwapa
"huwapa falme"
Belteshaza
Hili ni jina ambalo Wababeli walimpa Danieli.
anayeweza kunitafsiria
"wewe unaweza kuitafsiri ndoto"
roho ya miungu watakatifu
Nebukadneza aliamini kuwa nguvu za Danieli zilitoka kwa miungu ya uongo ambayo yey aliiabudu. Hii haina maana moja na "yey aliye mtakatifu" katika mstari wa 17.