sw_tn/dan/04/01.md

1.3 KiB

Maelezo ya jumla

Katika surahii, Nebukadneza anasema kile ambacho Mungu alimfanyia. Katika mistari ya 1-18, Nebukadneza anaeleza ndoto yake kwa nafsi ya kwanza. Katikamistari ya 19-33 anageuka na kutumia nafsi ya tatu katika kuelezea hukuma ya Nebukadneza. Mistari ya 34-37 anabadilika tena na kutumia nafsi ya kwanza katika kuelezea jibu lake kwa Mungu.

Mfalme Nebukadneza aliituma

Kirai hiki kinamrejelea mjumbe wa mfalme kana kwamba ni mfalme mwenyewe. "Mfalme aliwatuma wajumbe wake pamoja"

watu wote, mataifa, na lugha

"watu wote wa kila taifa na lugha"

walioishi katika nchi

Wafalme mara nyingi hutia chumvi kuhusu upana wa ufalme wao ulivyokuwa. Nebukadneza alitawala juu ya sehemu kubwa ya dunia inayojulikana katika kipindi ambacho kitabu hiki kiliandikwa.

amani yenu na iongezeke

Hii ni salaamu ya kawaida.

ishara na maajabu

Maneno haya yana maana sawa na yanarejelea vitu vya kushangaza ambavyo Mungu alikuwa amevifanya.

Ni kwa namna gani Ishara zake ni kubwa, na ni kwa namna gani maajabu yake

Virai hivi viwili vina maana moja na vimetumika katika kutia mkazo juu ya ukubwa wa ishara na maajabu ya Mungu yalivyo.

Ufalme wake ni ufalme unaodumu milele, na utawala wake hudumu kizazi hadi kizaz

Virai hivi vina maana moja na vimerudiwa ili kutia mkazo jinsi utawala wa Mungu ni wa milele.