sw_tn/2ki/16/03.md

1.3 KiB

akatembea katika njia ya wafalme wa Israeli

Kutembea inawakilisha tabia na matendo. "Mfalme Ahazi alitenda kama ambavyo wafalme wa Israeli walivyotenda" au "alifanya mambo ambayo wafalme wa Israeli waliyoyafanya"

kufuatana na machukizo yafanywayo na mataifa

Hapa "kufuata" inawakilisha yale wengine wafanyayo. "kunakili mambo maovu ambayo mataifa mengine wamefanya"

mataifa

Neno "mataifa" linawakilisha watu wa mataifa mengine. Hapa inarejea kwa watu wa mataifa waliokuwa wakiishi katika hiyo nchi. "watu wa mataifa mengine"

ambayo Yahwe aliwafukuza

"Kuwafukuza" inaamanisha "kuwatoa kwa nguvu." "ambao Yahwe aliwalazimisha kuondoka"

mbele ya watu wa Israli

Watu wa hayo mataifa walikimbia kama watu wa Israeli walivyoondoka kwenye nchi. "mbele ya watu wa Israeli waliondoka kwenye nchi" au "kama watu wa Israeli walivyoondoka kwenye nchi"

mahali pa juu, juu ya milima, na chini ya kila mti mbichi

Haya ni maeneo ambapo watu wa mataifa mengine walipoabudu miungu yao ya uongo.

chini ya kila mti mbichi

Mungu aliwataka watu wake kutoa sadaka kwake katika Yerusalimu. Neno "kila" hapa ni kutia chumvi kuonyesha jinsi Mfalme Ahazi alivyodhamiria kutokumtii Mungu kwa kutoa sadaka katika mahali pengine badala yake. "chini ya miti mingi mibichi" au "chini ya miti mingine izungukayo nchi"