sw_tn/2ki/08/18.md

1.2 KiB

Yehoramu akaenenda katika njia za wafalme wa Israeli

Hapa "kuenenda" ni lugha inayorejea jinsi alivyoishi na kutawala kama mfalme. Katika kipindi hiki kihistoria, wafalme wa Israeli walikuwa wafalme waovu. Maana halisi ya hii sentensi inaweza kuwekwa wazi. "Yehoramu alikuwa mfalme muovu, kama wafalme wengine wa Israeli waliotawala kabla yake alivotawala"

kama nyumba ya Ahabu ilivokuwa ikifanya

Hapa "nyumba" ya Ahabu inarejea kwa wadau wa familia ya Ahabu na uzao wake mpya. Ahabu ni mkwe wa Yoramu. "sawa kama familia iliyobaki ya Ahabu ilivyokuwa inafanya"

kwa kuwa alikuwa na binti wa Ahabu kama mkewe

Yehoramu alimuoa binti Ahabu.

alifanya yaliyo maovu usoni mwa Yahwe

Hapa "uso" wa Yahwe unarejea kwa yale ayafikiriyo. "alifanya mambo ambayo Yahwe aliyoyasema yalikuwa maovu"

angamiza Yuda

Hapa "Yuda" ni kielelezo kwa ajili ya watu walioishi huko. "angamiza watu wa Yuda"

tangu alipomwambia kwamba atampatia wazao

"tangu Yahwe alipomwambia Daudi kwamba angeupatia uzao wa Daudi." Hii inarejea kwa ahadi ya Yahwe kwa Daudi kwamba ukoo wake ungeitawala Yuda. Maana kamili ya hii sentence inaweza kuwekwa wazi. "tangu alipomwambia Daudi kwamba huu ni ukoo utakaoitawala Yuda.