sw_tn/1sa/08/06.md

486 B

Lakini haikumpendeza Sameli ... Utupatie mfalme

Samweli hakuwa na furaha kwamba watu hawakutaka yeye awaondoe watoto wake waliokuwa waovu na kumteua mwamuzi mwingine lakini walitaka mfalme wa kutawala juu yao kama nchi nyingine zinavyofanya.

Sikiliza sauti ya watu

Hapa neno "sauti" linamaana ya mapenzi au matakwa ya watu. "Fanya kama vile watu wanavyotaka"

bali wamenikataa mimi

Bwana alijua kuwa watu hawakuwakataa viongozi waovu tuu bali walimkataa yeye kama mfalme wao.