sw_ulb/52-COL.usfm

137 lines
12 KiB
Plaintext

\id COL
\ide UTF-8
\h Wakolosai
\toc1 Wakolosai
\toc2 Wakolosai
\toc3 col
\mt Wakolosai
\c 1
\cl Sura 1
\p
\v 1 Paulo, mtume wa Kristo Yesu kwa mapenzi ya Mungu, na Timotheo ndugu yetu,
\v 2 kwa watu watakatifu wa Mungu na ndugu waaminifu katika Kristo walioko Kolosai. Neema iwe kwenu, na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu.
\p
\v 3 Tunatoa shukrani kwa Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, na tunawaombea kila mara.
\v 4 Tumesikia imani yenu katika Yesu Kristo na upendo mlionao kwa watu wote watakatifu wa Mungu,
\v 5 kwa sababu ya taraja la uhakika lililohifadhiwa mbinguni kwa ajili yenuMlisikia kuhusu taraja hiyo ya uhakika katika neno la ukweli, injili
\v 6 ambayo imekuja kwenu. Na kwa njia hiyo hiyo, Injili hii inazaa tunda na inaenea ulimwenguni koteImekuwa ikifanya hivi ndani yenu tangu siku mlipoisikia na kufahamu neema ya Mungu katika kweli.
\v 7 Hii ndiyo injili kama mlivyojifunza kutoka kwa Epafra, mtumishi mwenzetuambaye ni mtumishi mwaminifu wa Kristo kwa ajili yetu.
\v 8 Epafra ameufanya ujulikane kwetu upendo wenu katika Roho.
\p
\v 9 Kwa sababu ya upendo huu, tangu siku tuliposikia hivi, hatujakoma kuwaombea. Tumekuwa tukiomba kwamba mtajazwa na maarifa ya mapenzi yake katika hekima yote na ufahamu wa kiroho,
\v 10 Tumekuwa tukiomba kwamba mtatembea kwa ustahimilivu wa bwana katika njia zipendezazo Bwana. Tumekua tukiomba mtazaa tunda katika kila tendo jema na kwamba mtakua katika maarifa ya Mungu.
\v 11 Tunaomba muweze kutiwa nguvu katika kila uwezo kulingana na nguvu za utukufu wakekatika uvumilivu na ustahimilivu wote.
\v 12 Tunaomba kwamba kwa furahamtatoa shukrani kwa Baba aliyewafanya ninyi mweze kuwa na sehemu katika urithi wa waumini katika nuru.
\p
\v 13 Ametuokoa kutoka katika utawala wa giza, akatuhamishia katika ufalme wa Mwana wake mpendwa.
\v 14 Katika mwanae tuna ukombozi na msamaha wa dhambi.
\v 15 Mwana ni mfano wa Mungu asiyeonekana, mzaliwa wa kwanza wa uumbaji wote.
\v 16 Kwa kuwa kwa yeye vitu vyote viliumbwa, vile vilivyoko mbinguni na vilivyoko duniani, vitu vinavyoonekana na visivyoonekana. Ikiwa ni vya enzi au mamlaka au utawala au wenye nguvu, vitu vyote viliumbwa na yeye na kwa ajili yake.
\v 17 Yeye amekuwepo kabla ya vitu vyote, na katika yeye vitu vyote vinashikamana pamoja.
\v 18 Na yeye ndiye kichwa cha mwili yaani kanisa, yeye ni mwanzo, na mzaliwa wa kwanza kutoka miongoni mwa wafu, hivyo, ana nafasi ya kwanza miongoni mwa vitu vyote.
\v 19 Kwa kuwa Mungu alipendezwa kwamba utimilifu wake wote uishi ndani yake,
\v 20 na kupatanisha vitu vyote kwake kwa njia ya Mwanawe. Mungu alifanya amani kupitia damu ya msalaba wake. Akapatanisha vitu vyote kwake mwenyewe, ikiwa ni vitu vya duniani au vitu vya mbinguni.
\p
\v 21 Nanyi pia, kwa wakati mmoja, mlikuwa mmetengwa na Mungu na mlikua maadui katika akili na matendo maovu.
\v 22 Lakini sasa amewapatanisha ninyi kwa mwili wake kupitia kifo. Alifanya hivi ili kuwaleta ninyi watakatifu, wasio na lawama na bila dosari mbele yake,
\v 23 kama mkiendelea katika imani, mliyoimarishwa na kuwa thabiti, pasipo kuondoshwa kutoka kwenye taraja la ujasiri la injili mliyoisikia. Hii ndiyo injili ambayo ilihubiriwa kwa kila kiumbe chini ya mbingu. Hii ndiyo injili ambayo kwayo mimi, Paulo, nimekuwa mtumishi.
\p
\v 24 Sasa nayafurahia mateso yangu kwa ajili yenu. Nami natimiliza katika mwili wangu kinachopungua kwa mateso ya Kristo kwa ajili ya mwili wake, ambao ni kanisa.
\v 25 Mimi ni mtumishi wa kanisa hili, sawasawa na wajibu niliopewa kutoka kwa Mungu kwa ajili yenu, kulitimiza neno la Mungu.
\v 26 Huu ni ukweli wa siri iliyofichwa kwa miaka mingi na kwa vizazi. Lakini sasa imefunuliwa kwa wote waaminio katika yeye.
\v 27 Ni kwa wale ambao Mungu alitaka kufunua ulivyo utajiri wa utukufu wa siri ya ukweli miongoni mwa Mataifa, Ni kwamba Kristo yumo ndani yenu, ujasiri wa utukufu ujao.
\v 28 Huyu ndiye tunayemtangaza. Tunamwonya kila mtu, na kumfundisha kila mtukwa hekima yote, ili kwamba tumlete kila mtu mkamilifu katika Kristo.
\v 29 Kwa ajili hii, mimi najibiidisha na kujitahidi kulingana na nguvu yake ifanyayo kazi ndani yangu katika uweza.
\c 2
\cl Sura 2
\p
\v 1 Kwa kuwa nataka mfahamu jinsi ambavyo nimekuwa na taabu nyingi kwa ajili yenu, kwa wote walioko Laodikia, na kwa wote ambao hawajauona uso wangu katika mwili.
\v 2 Nafanya kazi ili mioyo yao ifarijiwe, kwa kuletwa pamoja katika upendo na katika utajiri wote wa wingi wa uhakika kamili na maarifa, katika kuijua siri ya kweli ya Mungu, ambaye ni Kristo.
\v 3 Katika Yeye hazina zote za hekima na maarifa zimefichwa.
\v 4 Nasema hivi ili kwamba mtu yeyote asije akawadanganya kwa hotuba yeye ushawishi.
\v 5 Na ingawa sipo pamoja nanyi katika mwili, lakini nipo nanyi katika roho. Ninafurahi kuona utaratibu wenu mzuri na nguvu ya imani yenu katika Kristo.
\p
\v 6 Kama mlivyompokea Kristo Bwana, tembeeni katika yeye.
\v 7 Mwe na mzizi ndani yake, mjengwe katika yeye, mwimarishwe katika imani kama tu mlivyofundishwa, na kufungwa katika shukrani nyingi.
\p
\v 8 Angalieni ya kwamba mtu yeyote asiwanase kwa falsafa na maneno matupu ya udanganyifu kulingana na mapokeo ya wanadamu, kulingana na kanuni za kidunia, na sio kulingana na Kristo.
\v 9 Kwa kuwa katika yeye ukamilifu wote wa Mungu unaishi katika mwili.
\v 10 Nanyi mmejazwa katika yeye. Yeye ni kichwa cha kila uweza na mamlaka.
\v 11 Katika yeye pia mlitahiriwa kwa tohara isiyofanywa na wanadamu katika kuondolewa mwili wa nyama, lakini ni katika tohara ya Kristo.
\v 12 Mlizikwa pamoja naye katika ubatizo. Na kwa njia ya imani katika yeye mlifufuliwa kwa uweza wa Mungu, aliyemfufua kutoka kwa wafu.
\v 13 Mlipokuwa wafu katika makosa yenu na kutokutahiriwa kwa miili yenu, aliwafanya hai pamoja naye na kutusamehe makosa yetu yote.
\v 14 Alifuta kumbukumbu ya madeni iliyoandikwa, na taratibu zilizokuwa kinyume nasi. Aliiondoa yote na kuigongomea msalabani.
\v 15 Aliziondoa nguvu na wenye mamlakaAliyaweka wazi na kuyafanya kuwa sherehe ya ushindi kwa njia ya msalaba wake.
\p
\v 16 Kwa hiyo, mtu yeyote asiwahukumu ninyi katika kula au katika kunywa, au kuhusu siku ya sikukuu au mwezi mpya, au siku za Sabato.
\v 17 Hivi ni vivuli vya mambo yajayo, lakini kiini ni Kristo.
\v 18 Mtu awaye yeyote asinyang'anywe tuzo yake kwa kutamani unyenyekevu na kuabudu malaika. Mtu wa jinsi hiyo huingia katika mambo aliyoyaona na kushawishiwa na mawazo yake ya kimwili.
\v 19 Yeye hakishikilii kichwa. Ni kutoka katika kichwa kwamba mwili wote kupitia viungo vyake na mifupa huungwa na kushikamanishwa kwa pamoja; na hukua kwa ukuaji utolewao na Mungu.
\p
\v 20 Ikiwa mlikufa pamoja na Kristo kwa tabia za dunia, mbona mnaishi kama mnawajibika kwa dunia:
\v 21 “Msishike, wala kuonja, wala kugusa?”
\v 22 Haya yote yameamuriwa kwa ajili ya uharibifu ujao na matumizi, sawasawa na maagizo na mafundisho ya wanadamu.
\v 23 Sheria hizi zina hekima ya dini zilizotengenezwa kwa ubinafsi na unyenyekevu na mateso ya mwili. Lakini hazina thamani dhidi ya tamaa za mwili.
\c 3
\cl Sura 3
\p
\v 1 Ikiwa basi Mungu amewafufua pamoja na Kristo, yatafuteni mambo ya juu ambako Kristo anakaa mkono wa kuume wa Mungu.
\v 2 Fikirini kuhusu mambo ya juu, sio kuhusu mambo ya duniani.
\v 3 Kwa maana mlikufa na maisha yenu yamefichwa pamoja na kristo ndani ya mungu.
\v 4 Wakati kristo atakapoonekana, ambaye ni maisha yenu, ndipo nanyi pia mtakapoonekana, naye katika utukufu.
\p
\v 5 Kwa hiyo yafisheni mambo yaliyo katika nchi yaani, uasherati, uchafu, shauku mbaya, nia mbaya, na tamaa, ambayo ni ibada ya sanamu.
\v 6 Ni kwa ajili ya mambo haya ghadhabu ya Mungu inakuja juu ya wana wasio tii.
\v 7 Ni kwa ajili ya mambo haya ninyi pia mlitembea kwayo mlipoishi kati yao.
\v 8 Lakini sasa ni lazima myaondoe mambo haya yote. Yaani, ghadhabu, hasira, nia mbaya, matusi, na maneno machafu yatokayo vinywani mwenu.
\v 9 Msidanganyane ninyi kwa ninyi, kwa kuwa mmeuvua utu wenu wa kale na matendo yake.
\v 10 Mmevaa utu upya, unaofanywa upya katika maarifa sawasawa na mfano wa yule aliyeuumba.
\v 11 Katika maarifa haya, hakuna Myunani wala Myahudi, kutahiriwa wala kutokutahiriwa, msomi, asiye msomi, mtumwa, mtu huru, bali Kristo ni mambo yote katika yote.
\p
\v 12 Kama wateule wa Mungu, watakatifu na wapendwao, jivikeni utu wema, ukarimu, unyenyekevu, upole na uvumilivu.
\v 13 Chukulianeni ninyi kwa ninyi. Hurumianeni kila mtu na mwenzake. Kama mtu analalamiko dhidi ya mwingine, amsamehe kwa jinsi ileile ambayo Bwana alivyo wasamehe ninyi.
\v 14 Zaidi ya mambo haya yote, muwe na upendo, ambao ndio kigezo cha ukamilifu.
\p
\v 15 Amani ya Kristo itawale mioyoni mwenu. Ilikuwa ni kwa ajili ya amani hii mliitiwa katika mwili mmoja. Iweni na shukrani.
\v 16 Na Neno la Kristo likae ndani yenu kwa wingi. Kwa hekima yote, fundishaneni na kushauriana ninyi kwa ninyi kwa Zaburi katika hekima yote, mkimwimbia saburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni. Imbeni kwa shukrani mioyoni mwenu kwa Mungu.
\p
\v 17 Na chochote mfanyacho katika maneno au katika matendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu. Mpeni shukrani Mungu baba kupitia Yeye.
\p
\v 18 Wake, wanyenyekeeni waume zenu, kama ipendezavyo katika Bwana.
\v 19 Nanyi waume, wapendeni wake zenu, na msiwe wakali dhidi yao.
\p
\v 20 Watoto, watiini wazazi wenu katika mambo yote, maana ndivyo impendezavyo Bwana.
\v 21 Akina baba msiwachokoze watoto wenu, ili kwamba wasije wakakata tamaa.
\p
\v 22 Watumwa, watiini mabwana zenu katika mwili kwa mambo yote, sio kwa huduma ya macho kama wapendezao watu tu, bali kwa moyo wa kweli. Mcheni Mungu.
\v 23 Chochote mfanyacho, fanyeni kutoka nafsini mwenu kama kwa Bwana na si kama kwa wanadamu.
\v 24 Mnajua ya kwamba mtapokea ujira wa urithi kutoka kwa Bwana. Ni Kristo Bwana mnayemtumikia.
\v 25 Kwa sababu yeyote atendaye yasiyo haki atapokea hukumu kwa matendo yasiyo haki aliyoyafanya, na hakuna upendeleo.
\c 4
\cl Sura 4
\p
\v 1 Mabwana, toeni kwa watumwa mambo yaliyo haki na ya adili. Mnajua pia kwamba mnaye Bwana mbinguni.
\p
\v 2 Endeleeni kuwa thabiti katika maombi. Kaeni macho katika hilo kwa shukrani.
\v 3 Mkituombea pamoja pia, ili kwamba Mungu afungue mlango kwa ajili ya neno, kunena siri ya ukweli ya Kristo. Kwa sababu ya hili nimefungwa minyororo.
\v 4 Ombeni kwamba niweze kulweka wazi kama inavyonipasa kusema.
\p
\v 5 Enenda kwa hekima kwa wale walioko nje, na muukomboe wakati.
\v 6 Maneno yenu na yawe na neema wakati wote, na yakolee chumvi majira yote, ili kwamba mweze kujua jinsi inavyowapasa kumjibu kila mtu.
\p
\v 7 Kwa mambo yanayonihusu mimi, Tikiko atayafanya yajulikane kwenu. Yeye ni ndugu mpendwa, mtumishi mwaminifu, na mtumwa mwenzetu katika Bwana.
\v 8 Namtuma kwenu kwa ajili ya hili, kwamba mweze kujua mambo kuhusu sisi, na pia kwamba aweze kuwatia moyo.
\v 9 Namtuma pamoja na Onesimo, ndugu yetu mpendwa mwaminifu, na mmoja wenu. Watawaambia kila kitu kilichotokea hapa.
\p
\v 10 Aristarko, mfungwa mwenzangu, anawasalimu, pia na Marko binamu yake na Barnaba mliyepokea utaratibu kutoka kwake, “kama akija kwenu, mpokeeni,”
\v 11 Na pia Yesu aitwaye Yusto. Hawa peke yao wa tohara ni watendakazi wenzangu kwa ajili ya ufalme wa Mungu. Wamekuwa ni faraja kwangu.
\v 12 Epafra anawasalimu. Yeye ni mmoja wenu na mtumwa wa Kristo Yesu. Yeye hujitahidi siku zote katika maombi kwa ajili yenu ili kwamba mweze kusimama kwa ukamilifu na kuhakikishwa kikamilifu katika mapenzi yote ya Mungu.
\v 13 Kwa kuwa ninamshuhudia, kwamba anafanya kazi kwa bidii kwa ajili yenu, kwa hao walioko Laodekia, na kwa hao walioko Hierapoli.
\v 14 Luka yule tabibu mpendwa, na Dema wanawasalimu.
\p
\v 15 Wasalimu ndugu zangu walioko Laodekia, na Nimfa, na kanisa lile lililoko nyumbani kwake.
\v 16 Barua hii ikishasomwa kwenu, isomwe pia katika kanisa la walaodekia, nanyi pia hakikisheni mnaisoma ile barua kutoka Laodekia.
\v 17 Sema kwa Arkipo, “Angalia ile huduma ambayo umeipokea katika Bwana, kwamba unapaswa kuitimiza.”
\p
\v 18 Salamu hii ni kwa mkono wangu mwenyewe - Paulo. Ikuumbukeni minyororo yangu. Neema na iwe nanyi.