sw_tn/rom/06/12.md

1.4 KiB

Sentensi unganishi:

Paulo anatukumbusha sisi kwamba neema uongoza juu yetu, wala si sheria, sisi si watumwa wa dhambi, lakini watumwa wa Mungu.

msiache dhambi iwaongoze... Msiruhusu dhambi kuwaongoza

"Dhambi" inaelezwa kama mfalme wa mtu au bwana.

mwili wako wa kufa

Kikundi hiki cha maneno urejea kwa sehemu ya mwili wa mtu, ambayo utakufa. "wewe"

ili kusudi kwamba muweze kutii tamaa zake

Bwana. "dhambi" huitaji mwenye dhambi kutii amri za bwana kwa kufanya maovu.

Msitoe sehemu ya mwili wenu kwa dhambi kama vyombo vya udhalimu.

Hii picha ni ya mwenye dhambi anayetoa sehemu ya mwili wake kwa bwana wake au mfalme. "Msijitoe ninyi kwa dhambi ili kwamba msitende yasio faa."

lakini jitoeni kwa Mungu, kama walio hai kutoka kwenye mauti

"lakini jitoeeni ninyi kwa Mungu, kwa sababu amekwisha kuwapa ninyi maisha mapya ya kiroho"

sehemu ya miili yenu kama vyombo vya haki kwa Mungu

"acha Mungu akutumie kwa kile kimfurahisha cho yeye"

Msiruhusu dhambi kuwaongoza ninyi

"Msiache tamaa za dhambi kukuongoza kwa kile unachofanya" au "Usiruhusu wewe mwenyewe kufanya maovu unayotaka kufanya"

Kwa kuwa hamko chini ya sheria

Maana kamili inaweza kufanywa wazi. "kwa kuwa hamjafungamana na Sheria ya Musa, ambayo isingeweza kuwapa nguvu ya kuacha kufanya dhambi."

lakini chini ya neema

Maana kamili inaweza kufanywa wazi. "lakini mmefungamana na neema ya Mungu, ambayo inawapa nguvu ya kuacha kufanya dhambi."