sw_tn/mat/10/16.md

52 lines
1.8 KiB
Markdown

# Sentensi unganishi
Yesu anaendelea kuwaelekeza wanafunzi wake. Hapa anaanza kuwaambia wao kuhusu dhiki ambayo wanatakiwa kuvumilia pindi watapoenda kuhubiri.
# Angalia
Neno "Angalia" hapa linaongeza na kusisitiza ambacho kitafuatia. "Tazama"au "Sikiliza" au "Zingatia kile ninachotaka kukuambia"
# Ninawatuma
Yesu anawatuma kwa kusudi maalum.
# kama kondoo katikati ya mbwa mwitu
Kondoo ni wanyama wasioweza kuijhami ambao mara kwa mara hushambuliwa na mbwa mwitu. Yesu anasema kuwa watu wanaweza kuwaumiza wanafunzi wake. "Kama kondoo katikati ya mbwa mwitu hatari" au "kama kondoo katikati ya watu wenye tabia kama hizo.
# muwe na hekima kama nyoka na wapole kama njiwa
Yesu awaambia wanafunzi wake ili wawe na tahadhari na wasiowamiza watu. Kama kuwafananisha wanafunzi na nyoka au na njiwa kunachanganya, basi ni vizuri kutokuutumia huu mlinganyo. "fanya kwa kuelewa na tahadhari, vile vile kwa makini na wema."
# Muwe waangalifu na watu watawapeleka
Unaweza kutafsiri kwa kutumia "kwa sababu" ili kuonnesha jinsi hizi sentensi zinavyohusiana. "Muwe waangalifu na watu kwa sababu watawapeleka
# Watawapeleka kwenye
"watawasaliti kwa" au "watawakabidhi Kwa" au watawakamata na kuawajaribu"
# mabaraza
"mahakama" Hawa ni viongozi wa kidini au wazee ambao kwa pamoja wanalinda amani katika jamii.
# watawapiga mijeledi
"kupiga kwa mijeledi"
# katikati ya mbwa mwitu
AT:"katikati ya watu ambao ni kama mbwa mwitu wa hatari" au "katikati ya watu ambao watenda kama wanyama wa kutisha" au "katikati ya watu ambao watakuvamia wew"
# na mtaletwa
Hii inaweza kuelezeka katika muundo tendaji "watawaleta" au "watawaburuza"
# kwa ajili yangu
"kwasababu ninyi ni wangu" au "kwa sababu mnanifuata mimi"
# kwao na kwa mataifa
Kiwakilishi "kwao" inamaanisha huenda wakawa "magavana au wafalme" au kwa washitaki wa kiyahudi