sw_tn/lev/19/26.md

174 lines
4.2 KiB
Markdown

# damu
Msemo "damu" humaanisha kimiminika chekundu kinachotoka kwenye ngozi ya mtu panapokuwa na jeraha au kovu. Damu huleta virutubisho vitoavyo uhai kwa mwili mzima wa mtu.
* Damu hutoa ishara ya uhai na
inapomwagwa au kutolewa nje, hutoa
ishara ya kupoteza maisha, au kifo
* Watu waliotoa dhabihu kwa Mungu, waliua
mnyama na waliimimina damu yake juu ya
madhabahu. Hili lilitoa ishara ya dhabihu ya
uhai wa mnyama kulipa dhambi za mtu.
* Kwa kupitia kifo chake msabani, kiishara
damu ya Yesu iliwasafisha watu kutoka
katika dhambi zao na hulipa ile adhabu
wanayostari kwa ajili ya dhambi hizo
dhambi zao
* Yale maelezo "nyama na damu" humaanisha
wanadamu
* Yale maelezo "mwili na damu yako
mwenyewe" humaanisha watu
wanaohusiana kizazi
MAELEZO YA UFASIRI
* Msemo huu sharti ufasiriwe na msemo
unaotumika kwa damu katika lugha lengwa
* Yale maelezo "mwili na damu" yangeliweza
kufasiriwa kama "watu" au viumbe vyenye
uhai."
* Kulinga na muktatha, yale maelezo "nyama
na damua yangu mwenyewe "waweza
kufasiriwa kama "familia yangu mwenyewe"
au "jamaa yangu mwenyewe" au watu
wangu mwenyewe."
* Endapo kutakuwa na maelezo yoyote katika
lugha lengwa yanayotumika pamoja na
maana hii, yangeweza kufasiri "mwili na
damu"
# roho, -a kiroho
Msemo roho hulenga sehemu ya watu isiyo na maumbile isiyoweza kuonekana. Mtu anapokufa, roho yake huuacha mwili wake. Pia "roho" yaweza kumaanisha tabia au hali ya kujisikia.
* Ule msemo "roho" waweza kumaanisha
kiumbe kisicho na mwili unaoonekana,
hasa roho ovu.
* Roho ya mtu ni sehemu yake inayoweza
kumjua Mungu na kuamini katika Yeye.
* Kwa ujumla msemo "-a kiroho" hukielezea
chochote katika ulimwengu usio na
maumbile
* Kwenye Biblia, hasa hulenga chochote kile
kinachohusiana na Mungu, moja kwa moja
kwa Roho Mtakatifu.
* Kwa mfano, "chakula cha kiroho" huhusiana
na mafundisho ya Mungu yatoayo lishe kwa
roho ya mtu, "Ile "hekima ya kiroho"
humaanisha ufahamu na tabia adilifu
inayotokana na uweza wa Roho Mtakatifu.
* Mungu ni Roho naye aliumba viumbe roho
wengine wasio na miili ya kuonekana.
* Malaika ni viumbe roho, pamoja na wale
walioasi dhidi ya Mungu na wakawa roho
waovu.
* Ule msemo "roho ya" pia waweza
kumaanisha "kuwa na tabia bainishi za,"
kama vile katika, "roho ya hekima" au "katika roho ya Eliya."
* Mifano ya "roho" kama nia au hisia
ungejumuisha "roho ya woga" au "roho ya wivu"
MAPENDEKEZO YA UFASIRI
* Kwa kutegeana na muktadha, baadhi ya njia
za kufasiri "roho" zinaweza kuhusisha,
"kiumbe kisicho na maumbile" au "sehemu za
ndani" au "utu wa ndani."
* Katika mazingira mengine, ule msemo "roho"
waweza kufasiriwa kama "roho ovu" au
"kiumbe roho ovu"
* Wakati mwingine ule musemo "roho"
umetumika kuelezea hisia ya mtu aka vile,
"roho yangu ilihuzunishwa katika utu wangu
wa ndani." Hii pia yaweza kufasiriwa kama,
"nilijisikia kuhuzunishwa rohoni mwangu" au
"nilisikia kuhuzunishwa mno."
* Kile kirai roho ya" chaweza kufasiriwa kama,
"mwenendo wa, au ushawishi wa," au "nia ya"
au fikira"
# uweza, weuzo
Ule msemo "uweza" humaanisha uwezo wa kufanya mambo au kusababisha mambo yatokee, mara kwa mara kwa kutumia nguvu kubwa. "Uwezo" humaanisha watu au roho zenye uwezo wa kusababisha mambo kutokea.
* Ule "uweza" wa Mungu hurejelea uwezon
wa Mungu wa kufanya mambo yatokee,
hasa mambo yasiyowezekana kwa watu
kuyatenda.
* Mungu anauweza kamili juu ya kila kitu
ambacho amekiumba
* ungu huwapa watu wake uwezo wa
kufanya kile atakacho, ili kwamba
wanapoponya watu au kutenda miujiza,
wawe wanafanya hivi kwa uweza wa
Mungu.
MAPENDEKEZO YA UFASIRI
* Kwa kutegemeana na muktadha, ule
msemo "uweza" pia wawweza kufasiriwa
kama "uwezo" au "nguvu" au "bidii" au
"uwezo wa kutenda miujiza au kudhibiti."
* Njia zinazowezekana kufasiri msemo
"uweza" yaweza kuhusisha "wenye uhai
walio na uwezo mkubwa" au roho zenye
kutawala" au "wale wanaotawala wengine"
* Yale maelezo kama vile "utuokoe kutoka
katika nguvu za adui zetu" waweza
kufasiriwa kama, "utuokoe kutokana na
kugandamizwa na adui zetu" au "utuokoe
kutoka katika kutawaliwa na adui zetu."
Katika hali hii, "uweza" una maana ya
kutumia nguvu za mwingine kudhibiti na
kugandamiza wangine.