sw_tn/lev/08/30.md

6.3 KiB

Musa

Musa alikuwa nabii na kiongozi wa watu wa Musa alipokuwa mtoto, wasazi wake Musa walimweka kwennye kikapu kwenye mianzi ya mto Nile ili kumficha kutoka kwa Pharao wa Misri. Miriamu, dada yake Musa alimwangalia huko. Maisha ya Musa yalilindwa tu pale binti Farao alipomwona na kumpeleka ikulu kumlea kama mwanawe.

Mungu allimchagua Musa kuwaokoa Waisraeli kutoka utumwani Misri na kuwaongoza mpaka nchi ya ahadi.

Baada kuundoka kwa Waisraeli huko Misri, na wakiwa wanarunguka jangwani, Mungu alimpa Musa mbao mbili za mawe zilizoandikwa Amri za Mungu juu yake.

Karibu na mwisho wa uhai wake, Musa aliitazama tu nchi ya ahadi, lakini hakuingia kuishi humo kwa sababu hakumtii Mungu.

Paka mafuta, mpakwa mafuta

Neno "paka mafuta" humaanisha kusugua au mimina mafuta juu ya mtu au chombo, Wakati mwingine mafuta yalichanganywa na viungo, vikiyapa harufu yenye manukato. Neno pia limetumika kitamathari kumaanisha Roho Mtakatifu kumchaguwa na kumwezesha tu.

Katika Agano la Kale, makuhani, wafalme na manabii walipakwa mafuta ili kutenga kwa huduma maalum kwa Mungu.

Vyombo kama vile madhababhuau hema, vilipakwa mafuta kuonyesha kwamba vilikuwa vitumike kumwabudia na kumtukuza Mungu.

Katika Agano Jipya, wagonjwa walipakwa mafuta kwa uponyaji wao.

Agano Jipya hutaarifu mara mbili amabapo Yesu alipopakwa yenye manukato na wanawake, kama tendo la ibada. Wakati mmoja Yesu alisifia kwamba kwa kufanya hivi mwanamke huyo alikuwa akiandaa maziko Yake ya baadaye.

Yesu alipokufa, rafiki zake waliuandaa mwili wake kwa maziko kwa kuupaka mafuta na uvumba.

Vyeo "Mesiya" (Kiebrania) na "Kristo" (Kiyunani) humaanisha "Mpakwa mafuta"

MAPENDEKEZO YA UFASIRI

Kutegemeana na muktadha, neno "paka mafuta" laweza kufasiriwa kama "mimina mafuta juu ya" au "weka mafuta juu ya" au "weka wakfu kwa kumminia mafuta yaliyotiwa manukato."

"Kupakwa mafuta" laweza kufasiriwa kama "wekwa wakfu kwa kupakwa mafuta." au "teuliwa" au "wekwa wakfu."

Katika baadhi ya mazingira neno "paka mafutaa" linaweza kufasiriwa kama "teuwa."

Kirai kama "kuhani mpakwa mafuta," laweza kufasiriwa kama "kuhani aliyewekwa wakfu kwa mafuta" au kuhani aliyetengwa kwa miminiwa mafuta juu yake."

damu

Neno "damu" humaanisha kimiminika chekundu ambacho hutoka katika ngozi ya mtu kunapoukuwa na jeraha au kovu. Damu hutoa virutubisho viletavyo uhai katika mwili mzima wa mtu.

Damu huashiria uhai na inapomwagwa, huashiria kupoteza maisha au kifo.

Watu walipofanya dhabihu kwa Mungu, waliua mnyama na walimimina damu juu ya madhabahu. Hii iliifananisha dhabihu ya uhai wa damu ya mnyama

Mafuta

Mafuta ni kimiminika kizito, safi kilichotokana na mimea au matunda fulani. Kwa kawaida katika nyakati za Biblia yalitokana na mizeituni.

Mafuta ya zeituni yalitumika kwa kupikia, kupaka, dhabihu, taa, na dawa.

katika nyakati za kale, mafuta ya zeituni yalikuwa na gharama kubwa na umiliki wa mafuta ulihesabika kama kipimo cha utajiri.

Madhabahu

Madhabahu ni muundo ulionuliwa juu ambao juu yake Waisrali waliteketeza wanyama na nafaka kama sadaka kwa Mungu.

Nyakati za Biblia, mara kwa mara watu walitengeneza madhabahu rahisi kwa kuumba rundo la undongo uliofungashwa au kwa kupanga mawe makubwa kwa ungalifu ili kufanya rundo imara.

Baadhi ya madhabahu zilitengenezwa kwa kuunda makasha maalum kwa mbao zilizofunikwa kwa metali kama vile dhahabu, shaba nyeupe au shaba nyekundu.

Baadhi ya makundi mengine ya watu jirani na Israeli pia walijenga madhabahu ili kutoa dhabihu kwa miungu yao.

tenga

Neno "tenga" humaanisha kutengwa na jambo fulani ili kutimiza kusudi fulani.

Waisraeli walitengwa kwa huduma ya Mungu.

Roho Mtakatifu aliwaamru Wakristo wa Antiokia kuwatenga Paulo na Barnaba kwa kazi ya Mungu aliyowataka wao waifanye.

Mwamini "aliyetengwa" kwa kazi ya Mungu "amewekwa wakfu" kutimiza mapenzi ya Mungu.

Moja ya maana ya "mtakatifu" ni kutekwa kuwa wa Mungu na kuwa umetengwa kutoka katika njia za dhambi za ulimwengu.

Ule msamiati "takasa" humaanisha kumtenga mtu kwa huduma ya Mungu.

MAPENDEKEZO YA UFASIRI Njia za kufasiri "kutenga" zaweza kujumuisha, "kuchagua mahususi" au kutenga kutoka miongoni mwenu" au "kuweka kando ili kufanya kazi maalum."

"Kutengwa" kwaweza kufasiriwa "kuwekwa kando

Vaa, vikwa

Neno "kuvikwa na" linapotumika kitamathli kwenye Biblia, humaanisha kuruzukiwa au kuandaliwa kwa kitu fulani. "Kujivika" mwanyewe na kitu fulani humaanisha kutafuta kuwa na tabia yenye sifa fulani.

MAPENDEKEZO YA UFASIRI Kama inawezekana, ni vema kuitunza tamathali ya usemi, "jivike na." Njia nyingine ya kufasiri hili ni yaweza kuwa "vaa" kama hii ingemaanisha kuvaa nguo.

Kama hii haileti maana sahihi, njia nyingine ya kuifasiri tamathali "kuvikwa na" yaweza kuwa "kuonyesha" au "kudhihirisha" au kujazwa na" au kuwa na sifa ya."

Neno "jivike na" laweza pia kufsiriwa kama "jifunike na" au "enenda katika njia ambayo huonyesha."

mwana, mwana wa

Neno "mwana" hurejelea mvulana au katika uhusiano kwa wazazi. Laweza pia kumaanisha ama mzao mwanaume wa mtu fulani au kwa mwana aliyeasiliwa.

"Mwana," mara kwa mara limetumika kimafumbo katika Biblia kumaanisha mzao yeyote wa kiume, kama vile mjukuu au kitukuu.

Neno "mwana" pia linaweza kutumika kama muundo wa kistaraabu wa kumwita mvalana au mtu aliye kijana.

Wakati mwingine "wana wa Mungu" limetumika kwenye kumaanisha waaminio katika Kristo.

Mungu anaiita Israeli "mwanawe mzaliwa wa kwanza." Hii hurejelea uchaguzia wa Mungu wa taifa la Israeli kuwa watu maalum wa Mungu. Ni kwa kupitia kwao kwamba ujumbe wa ukombozi na wokovu ulikuja, ukiwa na matokeo yake kwamba watu wengi wamefanyika watoto wa kiroho.

Kirai "mwana wa" mara kwa mara limekuwa na maana ya kimafumbo, "kikiwa na sifa bainishi za." Mifono ya hiki hujumuisha wana wa nuru," "wana wa amani," na "wana wa ngurumo."

Kirai "mwana wa" pia kimetumika kuzungumzia ni nani aliye baba wa mtu. Kirai hiki hutumika kuelezea vizazi na maeneo mengine mengi.

Kwa kutumia "mwana wa" kwa kutoa jina la baba mara mara husaidia kutofautisha watu wenye majina yenye kufanana. Kwa mfano, "Azaria, mwana wa Sadoki" na Azaria, mwana wa katika 1 Wafalme 4, na "Azaria, mwana wa Amazia" katika 2 Wafalme 15 ni watu watatu waliotofauti.

MAPENDEKEZO YA UFASIRI Kwenye muktadha wa kukiri kwamba kitu fulani ni kweli, "kiri" laweza kufasiriwa kama "kubali" au "tangaza" au "ungama" kuwa ni kweli au "amini."

Linapomaanisha kumtambua mtu, neneo hili laweza kufasiriwa kama "pokea" au "tambua" uthamni wa" au ambia wengine kwamba