sw_tn/rev/front/intro.md

6.8 KiB

Utangulizi wa Ufunuo wa Yohana

Sehemu ya 1: Utangulizi wa jumla

Muhtasari wa Kitabu cha Ufunuo wa Yohana

  1. Mwanzo (1:1-20)
  2. Barua kwa makanisa saba (2:1-3:22)
  3. Maono juu ya Mungu akiwa mbinguni na maono ya Yule Mwanakondoo (4:1-11)
  4. Mihuri saba (6:1-8:1)
  5. Baragumu saba (8:2-13:18)
  6. Waabudu wa Mwanakondoo, wafia dini na mavuno ya hasira (14:1-20)
  7. Vitasa saba (15:1-18:24)
  8. Ibaada mbinguni (19:1-10)
  9. Hukumu ya Mwanakondoo, kuangamizwa wa yule mnyama, miaka elfu moja,kuangamizwa wa shetani na hukumu ya mwisho (20:11-15)
  10. Uumbaji upya na Yerusalemu mpya (21:1-22:5)
  11. Ahadi ya Yesu ya kurudi, ushuhuda wa malaika, maneno ya kumalizia ya Yohana, Ujumbe wa Kristo kwa kanisa,Mwaliko na onyo (22:6-21)

Nani aliandika kitabu cha Ufunuo wa Yohana?

Mwandishi anajitambulisha kama Yohana. Labda huyu ni Mtume Yohana. Aliandika kitabu cha Ufunuo akiwa katika kisiwa cha Patmosi. Warumi walikuwa wamempeleka huko kuishi uhamishoni kwa sababu ya kuwafundisha watu kumhusu Yesu.

Kitabu cha Ufunuo kinahusu nini?

Yohana aliandika kitabu cha Ufunuo kuwatia moyo waumini ili wabaki waaminifu ingawa walikuwa wanateseka. Yohana alifafanua maono aliyopata kumhusu shetani na wafuasi wake wakiwapinga na kuwaua waumini. Katika maono haya, Mungu anasababisha vitu vingi vibaya kutokea duniani na kuwaadhibu watu wabaya. Kwa mwisho Yesu anamshinda Shetani na wafuasi wake. Kisha Yesu anawafariji wale waliokuwa waaminfu. Na waumini wataishi milele pamoja na Mungu katika mbingu mpya na dunia mpya.

Kichwa cha kitabu hiki kinastahili kutafsiriwa namna gani?

Watafsiri wanaweza amua kukiita kitabu hiki na mojawapo wa vichwa vyake vya kitamaduni kama, "Ufunuo," "Ufunuo wa Yesu Kristo,"Ufunuo kwa Mtakatifu Yohana," ama "Apokalipi wa Yohana."Ama wanaweza kuchagua kichwa cha kueleweka zaidi kama "Vitu alivyovionyesha Yesu Kristo kwa Yohana." (Tazama: rc://*/ta/man/translate/translate-names)

Ni aina gani ya uandishi wa kitabu cha Ufunuo?

Yohana alitumia aina maalum ya uandishi kufafanua maono yake. Yohana anafafanua alichokiona kutumia alama nyingi. Mfumo huu wa uandishi unaitwa unabii wa alama ama fasihi ya kiapokalipti (inayozungumzia maangamizo yajayo). (Tazama: rc://*/ta/man/translate/writing-apocalypticwriting)

Sehemu ya 2: Dhana muhimu za kidini na kitamaduni

Je, matukio ya Ufunuo ni ya kipindi cha sasa ama kipindi kijacho?

Tangu wakati wa kwanza wa Ukristo, wasomi wamekuwa wakifafanua ufunuo tofauti. Wasomi wengine wanafikiri Yohana alifafanua matukio yaliyotokea nyakati zake. Wasomi wengine wanafikiri Yohana alifafanua matukio yaliyofanyika wakati wake hadi wakati Yesu atakaporudi. Wasomi wengine wanafikiri Yohana alifafanua matukio ambayo yangetokea muda mfupi kabla ya kurudi kwake Kristo.

Watafsiri hawatahitajika kuamua jinsi ya kukifafanua hiki kitabu hiki kitabu kabla ya kukitafsiri. Watafsiri waache unabii huo katika vitenzi vinavyotumika kwenye ULB.

Je, Kuna vitabu vingine kwenye Bibilia kama Ufunuo?

Hakuna kitabu kingine cha Bibilia kinachofanana na Ufunuo. Lakini aya katika vitabu vya Ezekieli, Zakaria na hasa Danieli zina mafundisho na aina sawa ya uandishi kama Ufunuo. Itakua na umuhimu kukitafsiri Ufunuo wakati sawa na Danieli kwa sababu vitabu hivi vina tamathali sawa za usemi na namna ya uandishi.

Sehemu ya 3: Maswala muhimu ya kitafsiri

Je, mtu anahitajika kukifahamu kitabu cha Ufunuo ili kukitafsiri?

Mtu hahitaji kufahamu alama zote katika kitabu cha Ufunuo ili kukitafsiri ipasavyo. Watafsiri wasitoe maana ya alama ama nambari katika tafsiri zao. (Tazama: rc://*/ta/man/translate/writing-apocalypticwriting)

Maswala ya "takatifu" na "takasa" yameakilishwa vipi katika Ufunuo ndani ya ULB?

Maandiko yanatumia maneno haya kuashiria mojawapo ya wawazo. Kwa sababu hii, ni vigumu kwa watafsiri kuyatumia vyema katika matoleo yao. Wakati wa kutafsiri Ufunuo kwa Kiingereza, ULB hufuata sheria zifuatazo:

  • Maana katika aya mbili inaashiria utakatifu wa kitabia. Hapa ULB inatumia "takatifu" (Tazama: 14:12; 22:11)
  • Mara nyingi maana yanaashiria Wakristo bila kufafanua majukumu watekelezayo. Katika hali kama hizi, ULB inatumia "Mwumini" ama "waumini". (Tazama:5:8; 8:3, 4; 11:18; 13:7; 16:6; 17:6; 18:20, 24; 19:8; 20:9)
  • Wakati mwingine maana yake inaashiria swala la mtu ama kitu kilichotengwa kwa ajili ya Mungu pekee. Katika hali kama hizi, ULB inatumia "takasa", "tenga kando", "kutabaruku kwa", ama "hifadhiwa kwa."

UDB itakuwa ya msaada kwa watafsiri kwa mara nyingi jinsi ya kuakiisha mawazo haya katika matoleo yao wenyewe.

Vipindi vya muda

Yohana aliashiria vipindi vingi vya muda katika Ufunuo. Kwa mfano kuna uashiriaji mwingi wa miezi arobaini na mbili, miaka saba, na miaka mitatu na nusu. Wasomi wengine wanafikiri vipindi hivi ni alama ya kitu fulani.Wasomi wengine wanafikiri kwamba hivi ni vipindi vya ukweli vya muda. Watafsiri wanatakikana kuvichukulia hivi vipindi kama vinavyoashiria vipindi kamili vya muda. Ni juu ya mtafsiri kuamua umuhimu wavyo ama vitu vinavyowakilishwa na vipindi hivi.

Ni maswala gani ya muhimu ya utafsiri katika kitabu cha Ufunuo?

Yafuatayo ni maswala muhimu ya uandishi katika Kitabo cha Ufunuo.

  • "Mimi ni alfa na omega,' asema Bwana Mungu, 'Yule aliye, na aliyekuwa, na atakayekuja, Mwenyezi'" (1:8). ULB,UDB na matoleo mengine ya kisasa husoma hivi. Matoleo mengine yanaongezea kauli "Mwanzo na Mwisho."
  • "Wazee wakasujudu wakaabudu" (5:14). ULB, UDB, na matoleo mengi ya kisasa yanasoma namna hivi. Matoleo mengine ya kale yanasoma, "Wale wazee ishirini na nne wakaanguka na kumwabudu yule anayeishi milele na milele."
  • "Mpaka sehemu ya tatu yake (dunia) ikachomeka" (8:7). ULB, UDB, na matoleo mengi ya kisasa yanasoma hivi.Matoleo mengine ya zamani hayana fungu hili la maneno.
  • Maandiko mengine yanaongezea fungu hili "na atakayekuja" (11:17). Lakini ULB, UDB na matoleo mengi ya kisasa hayafanyi hivyo.
  • Maanidko mengine yanaongezea fungu hili "mbele ya kiti cha enzi ya Mungu" (14:15)

lakini ULB, UDB na matoleo mengi ya kisasa hayafanyi hivyo."

  • "Aliyeko na aliyekuwepo, Yule Mtakatifu"16:5). ULB, UDB, na matoleo mengi ya kisasa yanasoma hivi. Matoleo mengine ya zamani yanasoma, "Ee Bwana, Yule aliye na aliyekuwa na atakayekuwa."
  • "Mataifa watatembea kwa mwanga wa jiji hilo" (21:24). ULB, UDB, na matoleo mengi ya kisasa husoma hivi. Matoleo mengine ya zamani husoma, "Mataifa yaliyookoka watatembea kwa mwanga wa "jiji hilo."
  • "Heri wazifuao nguo zao" (22:14). ULB, UDB, na matoleo mengi ya kisasa husoma hivi. Maandiko mengine ya zamani husoma hivi, "Heri wal wanaofuata amri zake."
  • "Mungu atamwondolea sehemu yake katika mti wa uzima na katika ule mji mtakatifu" (22:19).ULB, UDB, na matoleo mengi ya kisasa husoma hivi.Maandiko mengine ya kale husoma, "Mungu atachukua sehemu yake katika kitabu cha uzima na kwenye mji ule mtakatifu."

(See: rc://*/ta/man/jit/translate-textvariants)