sw_tn/php/front/intro.md

3.9 KiB

Utangulizi wa Wafilipi

Sehemu ya 1: Utangulizi wa jumla

Muhtasari wa kitabu cha Wafilipi

  1. Salamu,kushukuru na sala (1:1-11)

  2. Ripoti ya Paulo kuhusu huduma wake (1:12-26).

  3. Maelekezo

    • Kuwa imara (1:27-30)
    • Kuwa na umoja (2:1-2)
    • Kuwa na unyenyekevu (2:3-11)
    • Kutafuta wokovu wetu pamoja na Mungu akifanya kazi ndani yenu (2:12-13)
    • Kuwa bila hatia na kuwa na mwanga (2:14-18)
  4. Timotheo na Epafrodito (2:19-30)

  5. Onyo kuhusu walimu waongo (3:1-4:1)

  6. Maagizo ya kibinafsi(4:2-5)

  7. Uwe na furaha na usiwe na wasiwasi (4:4-6)

  8. Maneno ya mwisho

    • Maadili (4:8-9)
    • Kutosheka (4:10-20).

Nani aliandika kitabu cha Wafilipi?

Paulo aliandika Wafilipi. Paulo alitoka katika Mji wa Tarso. Hapo awali alijulikana kama Saulo. Alikuwa Mfarisayao kabla hajakuwa Mkristo. Aliwatesa sana Wakristo. Baada ya kuwa Mkristo, alisafiri sehemu nyingi katika ufalmwe ya Warumi akiwaambia watu kumhusu Yesu.

Paulo aliandika barua hii akiwa gerezani pale Roma.

Kitabu cha Wafilipi kinahusu nini?

Paulo aliwaandikia barua hii Waumini wa Filipi, mji ulioko Makedonia. Aliiandika kuwashukuru Wafilipi kwa zawadi waliomtumia. Alitaka kuwaelezea hali yake gerezani na kuwahimiza kuwa na furaha hata kama walikuwa wanateseka. Aliwaandikia pia kumhusu mtu mmoja aliyeitwa Epafrodito.Yeye ndiye aliyemplekea Paulo zawadi. Wakati akimpelekea zawadi, Epafrodito akawa mgonjwa.Kwa hivyo Paulo akaamua kumrudisha nyumbani Filipi. Paulo aliwahimiza waumini wa Filipi kumkaribisha na kumfanyia wema Epafrodito atakaporudi.

Kichwa cha kitabu hiki kinastahili kitafsiriwe namna gani?

Watafsiri wanaweza kukiita kitabu hiki jina lake la jadi,"Wafilipi." ama wanaweza kutumia kichwa kinachoeleweka zaidi kama "Barua ya Paulo kwa Kanisa la Filipi." ama "Barua kwa Wakristo walioko Filipi." (Tazama: rc://*/ta/man/translate/translate-names).

Sehemu ya 2: Maswala muhimu ya Kidini na Kitamaduni

Mji wa Filipi ulikuwa namna gani?

Filipi, baba yake Alekzanda Mkuu ndiye aliyeuanza mji wa Filipi katika eneo la Makedonia. Hii inamaanisha kwamba raia wa mji wa Filipi walichukuliwa kama raia wa Roma. Lakini Paulo akawaambia kwamba walikuwa raia wa mbinguni (3:20).

Sehemu ya 3: Maswala muhimu ya tafsiri

Umoja na wingi wa "nyinyi"

Kwenye kitabu hiki, Paulo anatumia neno "mimi' kumaanisha yeye. Neno "nyinyi" limetumika kama wingi na kumaanisha waumini wa Filipi. Mahali tu hii haizingatiwi ni 4:3(Tazama: [[rc:///ta/man/translate/figs-exclusive]] and [[rc:///ta/man/translate/figs-you]]).

Nani walikuwa "Maadui wa Msalaba wa Kristo" (3:18) katika barua hii?

Pengine "Maadui wa msalaba wa Kristo" walikuwa watu waliojiita waumini lakini hawakufuata maagizo ya Mungu. Walifikiri kwamba uhuru ndani ya Kristo ilimaanisha kwamba Waumini walikuwa huru kufanya wapendalo bila Mungu kuwaadhibu (3:19).

Ni kwa nini maneno "furahi" na "shangwe" yametumiwa mara nyingi katika barua hii?

Paulo alikuwa gerezani wakati aliandika barua hii (1:7). Ingawa alikuwa anateseka, Paulo alisema mara nyingi kwamba alifurahi kwamba Mungu alimpa wema kwa njia ya Kristo. Alitaka kuwahimiza wasomaji wake wawe na tumaini sawa na hilo kwa Yesu Kristo. (Tazama: rc://*/ta/man/translate/figs-irony)

Paulo anamaanisha nini kwa kauli "ndani ya kristo," "ndani ya Bwana," na kadhalika?

Aina hii ya maelezo inatokea katika 1:1,8,13,14,26, 27;2:1, 5, 19, 24, 29; 3:1, 3,9,14; 4:1,2, 4,7,10, 13, 19, 21. Paulo alitaka kuzungumzia hali ya Yesu kuwa karibu sana na waumini. Tazama utangulizi wa kitabu cha Warumi kwa maelezo zaidi.

Ni mambo gani muhimu zaidi katika maandishi ya kitabu cha Wafilipi?

  • Matoleo mengine yana "Amina" mwishoni mwa mstari wa mwisho katika barua hii (4:23). Matoleo ya ULB,UDB na mengine mengi ya kisasa hayana. Iwapo "Amina" imejumuishwa, basi lazima iwekwe katika alama ya mabano ya mraba ili kuonyesha kwamba siyo asili ya kitabu cha Wafilipi. (Tazama: rc://*/ta/man/jit/translate-textvariants)

(See: rc://*/ta/man/jit/translate-textvariants)