sw_tn/mrk/front/intro.md

6.5 KiB

Utangulizi wa injili ya Marko

Sehemu ya 1: Utangulizi wa Ujumla

Maelezo ya Kitabu cha Marko

  1. Utangulizi (1:1-13)

  2. Huduma ya Yesu huko Galilaya

    • Huduma ya awali (1:14-3:6)
    • Yesu anakuwa maarufu zaidi kati ya watu (3:7-5:43)
    • Kuondoka Galilaya na kurudi (6:1-8:26)
  3. Kuelekea Yerusalemu, nyakati mara nyingi ambapo Yesu anatabiri kifo chake mwenyewe; wanafunzi wanakosa kuelewa na Yesu anawafundisha jinsi itakuwa vigumu kumfuata (8:27-10:52)

  4. Siku za mwisho za huduma na maandalizi ya migogoro ya mwisho huko Yerusalemu (11:1-13-13:37)

  5. Kifo cha Kristo na kaburi tupu (14:1-16:8)

Je, kitabu cha Marko kinahusu nini?

Injili ya Marko ni moja ya vitabu vinne katika Agano Jipya ambavyo huelezea baadhi ya maisha ya Yesu Kristo. Waandishi wa Injili waliandika juu ya mambo mbalimbali kuonyesha kuwa Yesu alikuwa nani na ni nini alichofanya. Marko aliandika mengi juu ya jinsi Yesu aliteseka na kufa msalabani. Alifanya hivyo ili kuwatia moyo wasomaji wake ambao walikuwa wakiteswa. Marko pia alielezea desturi za Wayahudi na maneno mengine ya Kiaramu. Hii inaweza kuonyesha kwamba Marko alitarajia wengi wa wasomaji wake wa kwanza kuwa kuwa watu wa mataifa.

Je, kichwa cha kitabu hiki kinapaswa kutafsiriwaje?

Watafsiri wanaweza kuchagua kuita kitabu hiki kwa kichwa chake asilia, "Injili ya Marko" au "Injili Kulingana na Marko." Wanaweza pia kuchagua kichwa ambacho kinaweza kuwa wazi, kama vile "Habari Njema Kuhusu Yesu ambayo Marko Aliandika." (Angalia: rc://*/ta/man/translate/translate-names)

Nani aliandika Kitabu cha Marko?

Kitabo hakitupatia jina la mwandishi. Hata hivyo, tangu wakati wa Kikristo wa kwanza, Wakristo wengi wamefikiri kwamba mwandishi alikuwa Marko. Marko pia alijulikana kama Yohana Marko. Alikuwa rafiki wa karibu wa Petro. Marko huenda hakushuhudia kile Yesu alichosema na kufanya. Lakini wasomi wengi wanadhani kwamba Marko aliandika katika injili yake kile ambacho Petro alimwambia kuhusu Yesu.

Sehemu ya 2: Mawazo muhimu za Kidini na Kitamaduni

Je, ni njia zipi ambazo Yesu alitumia njia gani kwa kufundisha?

Watu walimwona Yesu kama rabi. Rabi ni mwalimu wa sheria ya Mungu. Yesu alifundisha kwa njia sawa na walimu wengine wa kidini huko Israeli. Alikuwa na wanafunzi ambao walimfuata kila mahali alipoenda. Wanafunzi hawa waliitwa wanafunzi. Mara nyingi aliwaambia mifano. Mifano ni hadithi zinazofundisha masomo ya maadili. (Angalia: [[rc:///tw/dict/bible/kt/lawofmoses]] na [[rc:///tw/dict/bible/kt/disciple]] na rc://*/tw/dict/bible/kt/parable)

Sehemu ya 3: Masuala muhimu ya Tafsiri

Je, vitabo vinavyoitwa sinoptiki ni vipi vya Injili ni vipi?

Vitabu vya Mathayo, Marko na Luka huitwa Injili za sinoptiki kwa sababu vina vifungu vingi vinavyofanana. Neno "synoptic" linamaanisha "kuona kwa pamoja."

Maandiko husemekana kuwa "sawa" wakati ambapo injili mbili au tatu zinafanana au zinakaribia kufanana. Wakati wa kutafsiri vifungu sambamba, wafasiri wanapaswa kutumia maneno sawa na kuyafananisha iwezekanavyo.

Je, kwa nini Yesu anajiita mwenyewe kama "Mwana wa Binadamu"?

Katika Injili, Yesu anajiita mwenyewe "Mwana wa Binadamu." Ni kumbukumbu ya Danieli 7:13-14. Katika kifungu hiki kuna mtu anayeelezewa kuwa "Mwana wa binadamu." Hiyo ina maana kwamba mtu huyo alifanana na mwanadamu. Mungu alitoa mamlaka kwa mwana wa binadamu kutawala mataifa milele. Na watu wote watamwabudu milele.

Wayahudi wa wakati wa Yesu hawakutumia "Mwana wa Binadamu" kama jina la mtu yeyote. Kwa hiyo, Yesu aliitumia kwa ajili yake mwenyewe ili kuwasaidia kuelewa yeye alikuwa nani kweli. (Angalia: rc://*/tw/dict/bible/kt/sonofman)

Kutafsiri jina "Mwana wa Binadamu" kunaweza kuwa vigumu kwa lugha nyingi. Huenda wasomaji hawaelewi tafsiri halisi. Watafsiri pia wanaweza kutumia jina mbadala, kama vile "Yule aliye Mtu." Inaweza pia kusaidia wanapoingiza maelezo ya chini ili kulielezea.

Je, kwa nini Marko mara nyingi hutumia maneno ambayo yanaashiria muda mfupi?

Injili ya Marko inatumia neno "mara moja" mara arobaini na mbili. Marko hufanya hivyo ili kufanya matukio kuwa ya kusisimua na ya wazi. Inamtoa msomaji haraka kutoka tukio moja hadi linalofuata.

Je, ni yapi masuala makuu katika maandishi ya Kitabu cha Marko?

Aya zifuatazo zinapatikana katika matoleo ya kale ya Biblia lakini hazijajumuishwa katika matoleo ya kisasa zaidi. Watafsiri wanashauriwa kutojumuisha aya hizi. Hata hivyo, ikiwa katika eneo la watafsiri, kuna matoleo ya zamani ya Biblia ambayo yanajumuisha moja au zaidi ya mistari hii, watafsiri wanaweza kuijumuisha. Ikiwa imejumuishwa, inapaswa kuwekwa ndani ya kifungo cha mraba ([]) ili kuonyesha kwamba labda asili yao haikuwa Injili ya Marko.

  • "Mtu yeyote aliye na masikio ya kusikia, na asikie." (7:16)
  • "ambapo mdudu wao hafi na moto hauzimiki" (9:44)
  • "ambapo mdudu wao hafi na moto hauzimiki" (9:46)
  • "Na maandiko yalitimizwa yaliyonena kwamba, 'Alihesabiwa pamoja na watu waovu'" (15:28)

Kifungu kinachofuata hakipatikani katika maandiko ya awali. Biblia nyingi zinajumuisha kifungu hiki, lakini Biblia za kisasa zimekiweka katika mabango ([]) au zinaonyesha kwa namna fulani kwamba kifungu hiki huenda si mfano ya kitabo cha asili cha Marko ya Injili ya Marko. Watafsiri wanashauriwa kufanya jambo sawa na matoleo ya kisasa ya Biblia.

  • "Mwanzoni mwa siku ya kwanza ya juma, baada ya kufufuka, alionekana kwanza kwa Maria Magdalene, ambaye alikuwa amemtoa pepo saba. Akaenda akawaambia wale waliokuwa pamoja naye, walipokuwa wanaomboleza na kulia. Walisikia kuwa alikuwa hai na kwamba yeye alikuwa amemwona, lakini hawakuamini. Baada ya hayo, Yesu alionekana kwa njia tofauti kwa wawili kati yao, walipokuwa wakitembea. Wakaenda kuwaambia wanafunzi wengine , lakini hawakuamini. Baadaye Yesu aliwatokea wale kumi na moja walipokuwa wameketi mezani, na akawakemea kwa kutoamini na ugumu wa moyo, kwa sababu hawakuamini wale waliomwona baada ya kufufuka kutoka kwa wafu. Akawaambia, 'Nendeni ulimwenguni kote, mkahubiri Habari Njema kwa viumbe vyote, yeye anayeamini na kubatizwa ataokolewa, na asiyeamini atahukumiwa. Ishara hizi zitawaongoza wale wanaoamini: Kwa jina langu watawatoa pepo. Watazungumza kwa lugha mpya. Watachukua nyoka kwa mikono yao, na ikiwa watakunywa kitu chochote cha mauti, hakitawaumiza. Wao wataweka mikono juu ya wagonjwWanafunzia, nao watapona.' Baada ya Bwana kuwazungumzia, alipelekwa mbinguni na akaketi kwenye mkono wa kuume wa Mungu. waliondoka na kuhubiri kila mahali, wakati Bwana alifanya kazi pamoja nao na kuthibitisha neno kwa ishara zilizowaongoza."(16:9-20)

(See: rc://*/ta/man/jit/translate-textvariants)