sw_tn/mat/front/intro.md

5.2 KiB

Utangulizi wa Injili ya Mathayo

Sehemu ya 1: Utangulizi wa Ujumla

Maelezo ya Kitabu cha Mathayo

  1. Kuzaliwa kwa Yesu Kristo na mwanzo wa huduma yake (1:1-4: 25)
  2. Mahubiri ya Yesu mlimani (5:1-7:28)
  3. Yesu anaonyesha ufalme wa Mungu kupitia matendo ya uponyaji (8:1-9:34)
  4. Mafundisho ya Yesu kuhusu utume na ufalme (9:35-10:42)
  5. Mafundisho ya Yesu kuhusu injili ya ufalme wa Mungu. Mwanzo wa upinzani kwa Yesu. (11:1-12: 50)
  6. Mifano ya Yesu kuhusu ufalme wa Mungu (13:1-52)
  7. Upinzani zaidi kwa Yesu na kutokuelewa kuhusu ufalme wa Mungu (13:53-17:57)
  8. Mafundisho ya Yesu kuhusu uhai katika ufalme wa Mungu (18:1-35)
  9. Yesu ahudumu katika Yudea (19:1-22:46)
  10. Mafundisho ya Yesu kuhusu hukumu ya mwisho na wokovu (23:1-25:46)
  11. Kusulubiwa kwa Yesu, kifo chake na ufufuo wake (26:1-28:19)

Je, kitabu cha Mathayo kinahusu nini?

Injili ya Mathayo ni moja ya vitabu vinne katika Agano Jipya ambavyo vinaelezea kuhusu maisha ya Yesu Kristo. Waandishi wa Injili waliandika juu ya mambo mbalimbali yaliyoonyesha kama Yesu alikuwa nani na ni nini alichofanya. Mathayo aliashiria kwamba Yesu alikuwa Masiya, na kama Mungu angeweza kuokoa Israeli kupitia kwake. Mathayo mara nyingi alielezea kwamba Yesu alitimiza unabii wa Agano la Kale kuhusu Masiya. Hii inaweza kuonyesha kwamba alitarajia kuwa wasomaji wake wengi wa kwanza watakuwa Wayahudi. (See: rc://*/tw/dict/bible/kt/christ)

Je, kichwa cha kitabu hiki kinapaswa kutafsiriwaje?

Watafsiri wanaweza kuchagua kukiita kitabu hiki kwa kichwa chake asilia, "Injili ya Mathayo," au "Injili kulingana na Mathayo." Au wanaweza kuchagua kichwa ambacho ni wazi, kama vile "Habari Njema ya Yesu ambayo Mathayo aliandika." (See: rc://*/ta/man/translate/translate-names)

Nani aliandika Kitabu cha Mathayo?

Kitabu hakitupi jina la mwandishi. Hata hivyo, tangu nyakati za hapo mwanzo za Kikristo, Wakristo wengi wamefikiri kwamba mwandishi alikuwa Mtume Mathayo.

Sehemu ya 2: Dhana muhimu za Kidini na za Kitamaduni

Je, "Ufalme wa mbinguni" ni nini?

Mathayo alizungumza juu ya ufalme wa mbinguni kwa njia ile ile ambayo waandishi wengine wa injili walizungumzia juu ya Ufalme wa Mungu. Ufalme wa mbinguni unawakilisha Mungu akitawala juu ya watu wote na viumbe vyote kila mahali. Wale ambao Mungu anakubali katika ufalme wake watabarikiwa. Wataishi pamoja na Mungu milele.

Je, njia za kufundisha za kufundisha zilikuwa zipi?

Watu walimwona Yesu kama rabi. Rabi ni mwalimu wa sheria ya Mungu. Yesu alifundisha kwa njia iliyokuwa sawa na njia ya walimu wengine wa kidini huko Israeli. Alikuwa na wanafunzi ambao walimfuata kila mahali alipoenda. Wanafunzi hawa waliitwa wanafunzi. Mara nyingi aliwaambia mifano. Mifano ni hadithi zinazofundisha masomo ya maadili. (See: [[rc:///tw/dict/bible/kt/lawofmoses]] and [[rc:///tw/dict/bible/kt/disciple]] na rc://*/tw/dict/bible/kt/parable)

Sehemu ya 3: Masuala muhimu ya Tafsiri

Je, vitabu vya kwanza vya Injili ni vipi?

Vitabu vya Mathayo, Marko na Luka huitwa injili za sinoptiki kwa sababu vina vifungu vingi vinavyofanana. Neno "sinoptiki" linamaanisha "kuona kwa pamoja."

Maandiko husemekana kuwa "sawa" wakati ambapo injili mbili au tatu zinafanana au zinakaribia kufanana. Wakati wa kutafsiri vifungu sambamba, wafasiri wanapaswa kutumia maneno sawa na kuyafananisha iwezekanavyo.

Je, kwa nini Yesu anajiita mwenyewe kama "Mwana wa Binadamu"?

Katika Injili, Yesu anajiita mwenyewe "Mwana wa Binadamu." Ni kumbukumbu ya Danieli 7:13-14. Katika kifungu hiki kuna mtu anayeelezewa kuwa "Mwana wa binadamu." Hiyo ina maana kwamba mtu huyo alifanana na mwanadamu. Mungu alitoa mamlaka kwa mwana wa binadamu kutawala mataifa milele. Na watu wote watamwabudu milele.

Wayahudi wa wakati wa Yesu hawakutumia "Mwana wa Binadamu" kama jina la mtu yeyote. Kwa hiyo, Yesu aliitumia kwa ajili yake mwenyewe ili kuwasaidia kuelewa kama yeye alikuwa nani. (See: rc://*/tw/dict/bible/kt/sonofman)

Kutafsiri jina "Mwana wa Binadamu" kunaweza kuwa vigumu kwa lugha nyingi. Labda wasomaji hawataelewa tafsiri halisi. Watafsiri pia wanaweza kutumia jina mbadala, kama vile "Yule aliye Mtu." Inaweza pia kusaidia wanapoingiza maelezo ya chini ya tanbihi ili kulielezea.

Je, ni yapi masuala makuu katika maandishi ya Kitabu cha Mathayo?

Haya ni masuala muhimu zaidi ya maandishi katika Kitabu cha Mathayo:

  • "Bariki wale wanaokulaani, tenda mema kwa wale wanaokuchukia" (5:44)
  • "Kwa maana ufalme ni wako na nguvu na utukufu milele. Amina" (6:13)
  • "Lakini aina hii ya pepo haitoki isipokuwa kwa maombi na kufunga" (17:21)
  • "Kwa maana Mwana wa Binadamu alikuja kuokoa kile kilichopotea" (18:11)
  • "Wengi huitwa, lakini wachache huchaguliwa" (20:16)
  • "Ole wenu, walimu wa Sheria na Mafarisayo, wanafiki! kwa kuwa mnaangamiza nyumba za wajane, wakati mnatoa sala ya muda mrefu. Basi mtapata hukumu kubwa zaidi." (23:14)

Watafsiri wanashauriwa kutoingiza vifungu hivi. Hata hivyo, ikiwa katika eneo la watafsiri, kuna matoleo ya zamani ya Biblia ambayo yanajumuisha moja au zaidi ya vifungu hivi, watafsiri wanaweza kuvijumuisha. Ikiwa vinajumuishwa, wanapaswa kuviweka ndani ya mabano ya mraba ([]) ili kuonyesha kwamba labda asili yao sio Injili ya Mathayo. (See: rc://*/ta/man/jit/translate-textvariants)