sw_tn/luk/front/intro.md

5.0 KiB

Utangulizi wa injili ya Luka

Sehemu ya 1: Utangulizi wa Ujumla

Maelezo ya Kitabu cha Luka

  1. Utangulizi na kusudi la kuandika (1:1-4)

  2. Kuzaliwa kwa Yesu na maandalizi ya huduma yake (1:5-4:13)

  3. Huduma ya Yesu huko Galilaya (4:14-9:50)

  4. Safari ya Yesu kwenda Yerusalemu

    • Ufuasi (9:51-11:13)
    • Migogoro na huzuni ya Yesu (11:14-14:35)
    • Mifano kuhusu vitu vilivyopotea na kupatikana. Mifano kuhusu uaminifu na udanganyifu (15:1-16:31)
    • Ufalme wa Mungu (17:1-19:27)
    • Kuingia kwa Yesu Yerusalemu (19:28-44)
  5. Yesu huko Yerusalemu (19:45-21:4)

  6. Mafundisho ya Yesu kuhusu kuja kwake mara ya pili (21:5-36)

  7. Kifo cha Yesu, kuzikwa kwake na ufufuo wake (22:1-24:53)

Je, kitabu cha Luka kinahusu nini?

Injili ya Yohana ni moja ya vitabu vinne katika Agano Jipya ambavyo huelezea baadhi ya maisha ya Yesu Kristo. Waandishi wa Injili waliandika juu ya mambo mbalimbali kuonyesha kuwa Yesu alikuwa nani na ni nini alichofanya. Luka aliandika injili yake kwa mtu aitwaye Theofilo. Luka aliandika maelezo sahihi ya maisha ya Yesu ili Theofilo awe na uhakika wa ukweli. Hata hivyo, Luka alitarajia injili kuwatia moyo waumini wote, si Theofilo tu.

Je, kichwa cha kitabu hiki kinapaswa kutafsiriwaje?

Watafsiri wanaweza kuchagua kuita kitabu hiki kwa kichwa chake asilia, "Injili ya Luka" au "Injili Kulingana na Luka." Au wanaweza kuchagua kichwa cha wazi zaidi, kama vile "Habari Njema Kuhusu Yesu "kama ilivyoandikwa na Luka." (See: rc://*/ta/man/translate/translate-names)

Nani aliandika Kitabu cha Luka?

Kitabu hiki hakitupatia jina la mwandishi. Aliyeandika kitabu hiki aliandika pia Kitabu cha Matendo. Katika sehemu zimoja za Kitabu cha Matendo, mwandishi hutumia neno "sisi." neno hili linaonyesha kuwa mwandishi huyu alisafiri na Paulo. Wasomi wengi wanadhani kwamba Luka alikuwa huyu mtu aliyesafiri na Paulo. Kwa hiyo, tangu nyakati za awali za Kikristo, Wakristo wengi walidhani kuwa Luka alikuwa mwandishi wa Kitabu cha Luka na Kitabu cha Matendo.

Luka alikuwa daktari. Uandishi wake unaonyesha kuwa alikuwa mtu wa elimu. Huenda alikuwa mtu wa mataifa. Labda Luka mwenyewe hakuhuhudia vile Yesu alivyosema na alivyofanya'. Lakini alisema kuwa alizungumza na watu wengi ambao walishuhudia matendo yake.

Sehemu ya 2: Dhana muhimu za Kidini na za Kitamaduni

Je, wanawake wana majukumu gani katika Injili ya Luka?

Luka aliwaelezea wanawake kwa njia nzuri sana katika injili yake. Kwa mfano, mara nyingi alionyesha wanawake kuwa waaminifu zaidi kwa Mungu kuliko wanaume wengi. (See: rc://*/tw/dict/bible/kt/faithful)

Kwa nini Luka anaandika mengi kuhusu wiki ya mwisho ya maisha ya Yesu?

Luka aliandika mengi juu ya wiki ya mwisho wa Yesu. Alitaka wasomaji wake kufikiri sana juu ya wiki ya mwisho wa Yesu na kifo chake msalabani. Aliwataka watu kuelewa kwamba Yesu kwa hiari alikufa msalabani ili Mungu awasamehe kwa ajili ya dhambi. (See: rc://*/tw/dict/bible/kt/sin)

Sehemu ya 3: Masuala muhimu ya Tafsiri

Je, vitabu vya sinoptiki vya Injili ni vipi?

Vitabu vya Mathayo, Marko na Luka huitwa injili za sinoptiki kwa sababu vina vifungu vingi vinavyofanana. Neno "synoptic" linamaanisha "kuona kwa pamoja."

Maandiko husemekana kuwa "sawa" wakati ambapo injili mbili au tatu zinafanana au zinakaribia kufanana. Wakati wa kutafsiri vifungu sambamba, wafasiri wanapaswa kutumia maneno sawa na kuyafananisha iwezekanavyo.

Je, kwa nini Yesu anajiita mwenyewe kama "Mwana wa Binadamu"?

Katika Injili, Yesu anajiita mwenyewe "Mwana wa Binadamu." Ni kumbukumbu ya Danieli 7:13-14. Katika kifungu hiki kuna mtu anayeelezewa kuwa "Mwana wa binadamu." Hiyo ina maana kwamba mtu huyo alifanana na mwanadamu. Mungu alitoa mamlaka kwa mwana wa binadamu kutawala mataifa milele. Na watu wote watamwabudu milele.

Wayahudi wa wakati wa Yesu hawakutumia "Mwana wa Binadamu" kama jina la mtu yeyote. Kwa hiyo, Yesu aliitumia kwa ajili yake mwenyewe ili kuwasaidia kuelewa yeye alikuwa nani. (See: rc://*/tw/dict/bible/kt/sonofman)

Kutafsiri jina "Mwana wa Binadamu" kunaweza kuwa vigumu kwa lugha nyingi. Wasomaji wana uwezo wa kutoelewa tafsiri halisi. Watafsiri pia wanaweza kutumia jina mbadala, kama vile "Yule aliye Mtu." Inaweza pia kusaidia wanapoingiza maelezo ya chini ili kulielezea.

Je, ni yapi masuala makuu katika maandishi ya Kitabu cha Luka?

Hizi ndizo masuala muhimu sana katika Kitabu cha Luka:

  • "Kisha malaika kutoka mbinguni akamtokea, akamtia nguvu. Kwa kuwa alikuwa na uchungu, aliomba kwa bidii zaidi, na jasho lake likawa kama matone makubwa ya damu yaliyodondoka chini. " (22:43-44) ULB na UDB hujumuisha kifungu hiki, lakini baadhi ya matoleo mengine hayana.
  • "Yesu akasema," Baba, wasamehe, kwa maana hawajui wanayofanya. "(23:34) ULB na UDB hujumuisha kifungu hiki, lakini baadhi ya matoleo mengine hayana.

Kifungu kinachofuata hakijaingizwa katika matoleo mengi ya kisasa. Matoleo mengine yanaiweka kwenye mabano ya mraba:

  • "Kwa maana alipaswa kumfungua mfungwa mmoja wakati wa sikukuu" (23:17)

(See: rc://*/ta/man/jit/translate-textvariants)