sw_tn/jhn/front/intro.md

5.2 KiB

Utangulizi wa injili ya Yohana

Sehemu ya 1: Utangulizi wa Ujumla

Maelezo ya Injili ya Yohana

  1. Utangulizi kuhusu Yesu ni nani (1:1-18)

  2. Yesu anabatizwa, na kuwachagua wanafunzi kumi na wawili (1:19-51)

  3. Yesu anahubiri, anafundisha, na kuwaponya watu (2-11)

  4. Siku saba kabla ya kifo cha Yesu (12-19

    • Maria anapaka mafuta miguu ya Yesu (12:1-11))
    • Yesu anampanda punda kwenda Yerusalemu (12:12-19)
    • Baadhi ya watu wa Kiyunani wanataka kumwona Yesu (12:20-36)
    • Viongozi wa Kiyahudi wanamkataa Yesu (12:37-50)
    • Yesu anawafundisha wanafunzi wake (13-17)
    • Yesu anakamatwa na kujaribiwa (18:1-19: 15)
    • Yesu anasulubiwa na kuzikwa (19:16-42)
  5. Yesu anafufuka (20:1-29)

  6. Yohana anasema kwa nini aliandika injili yake (20:30-31)

  7. Yesu anakutana na wanafunzi (21)

Je, kitabu cha Yohana kinahusu nini?

Injili ya Yohana ni moja ya vitabu vinne katika Agano Jipya ambavyo huelezea baadhi ya maisha ya Yesu Kristo. Waandishi wa Injili waliandika juu ya mambo mbalimbali kuonyesha kuwa Yesu alikuwa nani na ni nini alichofanya. Yohana alisema kwamba aliandika injili yake "ili watu waweze kuamini kwamba Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai" (20:31).

Injili ya Yohana ni tofauti kabisa na Injili nyingine tatu. Yohana hajumuishi baadhi ya mafundisho na matukio ambayo waandishi wengine walijumuisha katika injili zao. Pia, Yohana aliandika juu ya baadhi ya mafundisho na matukio ambazo hazipo katika injili nyingine.

Yohana aliandika mengi juu ya ishara alizofanya Yesu ili kuthibitisha kwamba kile Yesu alisema juu yake mwenyewe ni kweli. (See: rc://*/tw/dict/bible/kt/sign)

e, kichwa cha kitabu hiki kinapaswa kutafsiriwaje?

Watafsiri wanaweza kuchagua kuita kitabu hiki kwa kichwa chake asilia, "Injili ya Yohana" au "Injili kama ilivyoandikwa na Yohana." Au wanaweza kuchagua kichwa ambacho kinaweza kuwa wazi, kama vile "Habari Njema Kuhusu Yesu ambayo Yohana Aliandika." (See: rc://*/ta/man/translate/translate-names)

Nani aliandika Kitabu cha Yohana?

Kitabu hiki hakitupi jina la mwandishi. Hata hivyo, tangu wakati wa Kikristo wa kwanza, Wakristo wengi wamefikiri kwamba Mtume Yohana ndiye aliyekuwa mwandishi.

Sehemu ya 2: Dhana muhimu za Kidini na za desturi

Kwa nini Yohana anaandika mengi kuhusu wiki ya mwisho ya maisha ya Yesu?

Yohana aliandika mengi kuhusu wiki ya mwisho ya Yesu. Alitaka wasomaji wake kufikiri sana juu ya wiki ya mwisho ya Yesu na kifo chake msalabani. Alitaka watu waelewe kwamba Yesu kwa hiari alikufa msalabani ili Mungu awasamehe kwa ajili ya kutenda dhambi. (See: rc://*/tw/dict/bible/kt/sin)

Sehemu ya 3: Masuala muhimu ya Tafsiri

Maneno "kubaki," "kuishi," na "kukaa" yana maana gani katika injili ya Yohana?

Mara nyingi Yohana alitumia maneno "kubaki," "kuishi", na "kukaa" kama mifano. Yohana alizungumuza juu ya mwamini kuwa mwaminifu zaidi kwa Yesu na kumjua Yesu vizuri kama neno la Yesu "lilibaki" ndani ya yule mwamini. Pia, Yohana alizungumuza juu ya aliyejiunga kiroho na mtu mwingine kwa kusema "alibaki" ndani yake. Wakristo wanasema "kubaki" katika Kristo na kwa Mungu. Baba anasemwa "kubaki" ndani ya Mwana, na Mwana anasemwa "kubaki" ndani ya Baba. Mwana anasemwa "kubaki" katika waumini. Roho Mtakatifu pia anasemwa "kubaki" ndani ya waumini.

Watafsiri wengi wataona vigumu kwa kutafsiri mawazo hayo katika lugha zao kusema maneno sawasawa kabisa. Kwa mfano, Yesu alitaka kuelezea wazo la Mkristo kuwa kiroho pamoja naye wakati aliposema, "Yeye anayekula mwili wangu na kunywa damu yangu anakaa ndani yangu, na mimi ndani yake" (Yohana 6:56). UDB hutumia wazo la "ataunganishwa na mimi, nami nitaunganishwa naye." Lakini watafsiri wanaweza kutumia maneno nyingine za kueleza wazo hilo.

Katika kifungu hicho, "Ikiwa maneno yangu yanakaa ndani yenu" (Yohana 15:7), kulingana na UDB wazo hili linatafsiriwa kama, "Ikiwa unaishi katika ujumbe wangu." Watafsiri wanaweza kutumia tafsiri hii kama mfano.

Je, kuna maswali makuu gani katika maandishi ya Kitabu cha Yohana?

Haya ni masuala muhimu zaidi ya maandishi katika Kitabu cha Yohana:

  • "wakingoja maji kuchemka. Malaika wa Bwana mara na mara alishuka ndani ya bwawa na kuchochea mara na mara." (5:3-4)

Watafsiri wanashauriwa kutotafsiri kifungu hiki. Hata hivyo, ikiwa katika eneo la watafsiri, kuna matoleo ya zamani ya Biblia ambayo yanajumuisha kifungu hiki, basi watafsiri wanaweza kukijumuisha. Ikiwa inatafsiriwa, inapaswa kuwekwa ndani ya mabano ya mraba ([]) ili kuonyesha kwamba labda asili yake sio Injili ya Yohana. (See: rc://*/ta/man/jit/translate-textvariants)

  • Habari ya mwanamke mzinzi (7:53-8:11)

Kifungu hiki kinajumuishwa katika matoleo mengi ya kale na ya kisasa ya Biblia. Lakini hakiko katika nakala za kwanza za Biblia. Watafsiri wanashauriwa kutafsiri kifungu hiki. Kinapaswa kuwekwa ndani ya mabano ya mraba ([]) kuonyesha kwamba labda asili yake sio Injili ya Yohana. (See: rc://*/ta/man/jit/translate-textvariants)

  • Baadhi ya matoleo ya zamani pia yana kifungu hiki:

"kupitia katikati yao, na hivyo kupitia" (8:59)

Lakini ni hakika kwamba kifungu hiki hakikuwa hapo awali kwa Injili ya Yohana. Hakipaswi kuingizwa. (See: rc://*/ta/man/jit/translate-textvariants)

(See: rc://*/ta/man/jit/translate-textvariants)