sw_tn/col/front/intro.md

5.8 KiB

UTANGULIZI WA WAKOLOSAI

Sehemu ya 1: Utangulizi kwa ujumla

Muhtasari ya kitabo cha Wakolosai

  1. Salamu, kushuhuru na sala (1:1-12)

  2. Yesu na kazi yake

    • Wokovu na ukombozi (1:13-14)
    • Kristu: Taswira ya Mungu asiyeonekana, na Yule asimamiye vyote vilivyoumbwa(1:15-17)
    • Kristu ndiye kichwa cha kanisa na kanisa linamwamini (1:18-2:7)
  3. Majaribu ya uaminifu

    • Maonyo kuhusu walimu wapotovu (2:8-19)
    • Utiifu wa Mungu siyo sheria kali ama mila zisizovunjika (2:20-23)
  4. Mafunzo na maisha

    • Maisha katika Kristu (3-14)
    • Maisha ya kale na ya kisasa (3:5-17)
    • Familia ya Kikristo (3:18-4:1)
  5. Tabia ya Kikristo (4:2-6)

  6. Kumalizia na salamu

    • Paulo anamshukuru Tikiko na Onesimo (4:7-9)
    • Paulo anatuma salamu kutoka kwa washirika wake (4:10-14)
    • Paulo anatoa mwelekeo kwa Arkipo na Wakristu wa Laodikia (4:15-17).
    • Salamu za kibinafsi za Paulo (4:18)

Nani aliandika kitabu cha Wakolosai?

kitabu cha Wakolosai kiliandikwa na Paulo.Paulo alitoka katika mji wa Tarso. Hapo awali alijulkana kama Saulo. Kabla ya kuwa Mkristo, Paulo alikuwa Mfarisayo. Aliwatesa Wakristo. Baada ya kuwa Mkristo, alisafiri mara nyingi katika eneo lote la ufalme wa Warumi akiwahubiria watu kumhusu Yesu.

Paulo aliandika barua hii akiwa jela la Roma.

Kitabu cha Wakolosai kinahusu nini?

Paulo aliandika waraka huu kwa waumini wa Asia Ndogo walioko katika jiji la Kolosai. Lengo kuu la barua hii ni kuittetea injili kutokana na walimu wa uongo. Alifanya hivi kwa kumsifu Yesu kama taswira ya Mungu, anayekidhi vitu vyote na kuwa mkuu wa Kanisa. Paulo alitaka wafahamu kwamba Kristo ndiye alyehitajika ili wakubaliwe na Mungu.

Kichwa cha Kitabu hiki kitafsiriwe namna gani?

Watafsiri wanaweza amua kukiita kitabu hiki na jina lake la asili, "Wakolosai," ama wanaweza kutumia kichwa cha kueleweka zaidi kama "Barua ya Paulo kwa kanisa la Kolosai", ama "Barua kwa Wakristo wa Kolosai." (Tazama: rc://*/ta/man/translate/translate-names).

Sehemu ya 2: Maswala muhimu ya kidini na Kitamaduni

Maswala gani ya kidini yalitatanisha kanisa la Kolosai?

Kanisa la Wakolosai lilkuwa na walimu wa uongo. Mafundisho yao kamili hayajulikani. Kuna uwezekano waliwafundisha wafuasi wao kuwaabudu malaika na kufuata sheria kali za sherehe za kidini.Kuna uwezekano mkubwa kwamba walifundisha kwamba lazima wanaume watahiriwe na pia kuepuka aina fulani za chakula. Paulo pia alisema kwamba mafundisho ya uongo pia yalitoka kwa akili ya watu na siyo Mungu.

Paulo alitumiaje istiara ya mbingu na nchi?

Kwenye waraka huu, Paulo amezungumzia mara nyingi mbingu kama iliyo juu akiitofautisha na ardhi inayozungumziwa kama iliyo chini. Lengo la istiara hii ni kufundisha Wakristo waishi kwa njia inayomheshimu Mungu aishie juu mbinguni. Paulo hafundishi kwamba dunia hii iliyeumbwa ina uovu. (Tazama: rc://*/tw/dict/bible/kt/evil).

Sehemu ya 3: Maswala muhimu ya Tafsiri

Namuna gani Maswala ya 'takatifu' na 'kutakasa' yamewakilishwa katika Wakolosai ndani ya ULB?

Maandiko yanatumia maneno haya kuashiria baadhi ya maswala mengi. Kwa sababu hii ni vigumu kwa Watafsiri kuyawakilisha vema katika matoleo yao. Katika Wakolosai, maneno haya hutumika kuashiria WaKristo bila kuelezea majukumu yao. Kwa hivyo Wakolosai katika ULB hutumia "Waumini" ama "Walio na imani ndani yake." (Tazama: 1:2,12,26).

Je, Yesu aliumbwa ama alikuwepo tangu mwanzo?

Yesu hakuumbwa lakini amekuwa akiishi kama Mungu.Yesu pia alichukua umbo la binadamu. Kuna uwezekano mkuu wa kutatanisha katika Wakolosai 1:15 inayosema " Yeye ndiye mzaliwa wa kwanza wa viumbe wote."Kauli hii inamaanisha kwamba Yesu ni mkuu kwa vyumbe wote. Haimaanishi kwamba Yesu ndiye kiumbe wa kwanza kuumbwa na Mungu. Watafsiri wawe makini wasimaanishe Yesu ni kiumbe.

Paulo anamaanisha nini na maelezo "ndani ya Kristo,"Ndani ya Bwana," na kadhalika?

Paulo alitaka kueleza juu ya muungano wa karibu sana kati ya Kristo na waumini. Angalia utangulizi wa kitabo cha Waroma kwa maelezo mengine kuhusu maneno haya.

Ni maswala gani muhimu katika maandishi ya kitabu cha Wakolosai?

Matoleo mengine ya kisasa yanatofautina na ya kale kwenye mistari ifuatayo. Toleo la ULB lina maandishi ya kisasa na imeweka maandishi ya kale kama maelezo ya chini ya tanbihi.Iwapo kuna Biblia katika eneo kwa ujumla, watafsiri wanafaa kuamua kutumia maandishi kwenye matoleo hayo. Kama sivyo, watafsiri wanashauriwa kufuata maandishi ya kisasa.

  • "Tunawatakia neema na amani kutoka kwa Mungu Baba wetu" (1:2). Matoleo ya zamani yana maandishi marefu: "Neema na amani kutoka kwa Baba yetu Mungu na Bwana wetu Yesu Kristo viwe nanyi."
  • "Epafra, Mtumishi mwenzetu mpendwa, ambaye ni mtumishi mwaminifu wa Kristu kwa niaba yetu"(1:7). Matoleo mengine ya kale yanasema "kwa ajili yenu": Epafra, Mtumishi wetu mpendwa, Mtumishi mwaminifu wa Christu kwa ajili yenu."
  • "Baba aliyewafanya mustahili kushiriki uridhi wa waumini walio kwa mwanga.(1:12). Matoleo mengine ya zamani yanasoma, "Baba,aliyetuwezesha kushiriki katika mwanga wa uridhi."
  • "Katika Mwanawe tumepata ukombozi"(1:14). Matoleo mengine ya kale yanasema, "Katika Mwanawe tumepata ukuombozi katika damu yake."
  • "na akatusamehe dhambi zetu zote"(2.13). Matoleo mengine ya zamani yanasoma: "na akawasamehe dhambi zenu zote."
  • "Kristu, uhai wako, atakapotokea"(3:4). Matoleo mengine ya zamani yanasema, "Kristo, uhai wetu, atakapotokea."
  • "Ni kwa sababu ya mambo haya ndipo hasira ya Mungu inakuja kwa wana wasiotii" (3:6). Matoleo ya ULB,UDB ,na mengineyo ya kisasa husema hivi. Hata hivyo, kuna baadhi ya matoleo ya kisasa na ya kale ambayo husema, " Ni kwa sababu ya mambo haya ndipo hasira ya Mungu inakuja."
  • 'Ni kwa sababu ya haya mambo nikamtuma kwenu ili myafahamu mambo kutuhusu sisi"(4:8). Matoleo mengine yanasem, "Nilimtuma kwenu "ili ayafahamu mambo kuhusu nyinyi."

(See: rc://*/ta/man/jit/translate-textvariants)