sw_tn/job/03/20.md

40 lines
1.6 KiB
Markdown

# Kwa nini yeye aliye mashakani kupewa mwanga? Kwa nini hao wenye uchungu moyoni kupewa uhai
Maswali mawili ya Ayubu kimsingi humaanisha kitu kimoja. Yeye anashangaa kwanini hao ambao hukabili magumu huendelea kuishi.
# Kwa nini yeye aliye mashakani kupewa mwanga?
Hapa Ayubu anashangaa kwanini lazima watu wabaki hai na kuteseka. "Mimi sielewi kwa nini Mungu hutoa uhai kwa mtu ambaye anateseka"
# mwanga
Hapa mwanga unawakilisha uhai
# Kwa nini hao wenye uchungu moyoni kupewa uhai ... hazina iliyofichika?
"je kwa nini Mungu hutoa uhai kwa mtu mwenye taabu? "Mimi sielewi kwa nini Mungu anatoa uhai kwa mtu mwenye huzuni sana ... hazina iliyofichika"
# ambao hutamani mauti lakini hawapati
Hapa kifo kinazungumziwa kana kwamba kuna kitu kinakuja kikimwelekea mtu fulani. "kwa mtu ambaye haitaji tena kuwa hai, lakini bado yu-hai"
# ambao huyachimbulia mauti zaidi ya kutafuta hazina iliyofichika
Mtu anayetumainia kufa anazumgumziwa hapa kana kwamba anachimbua hazina iliyozikwa. "kwa mtu ambaye anahitaji kufa zaidi ya yeye kutafuta hazina iliyofichika"
# Kwa nini kupewa mwanga ambao hushangilia mno na kufurahi walionapo kaburi
Hapa Ayubu anatumia swali kufanya kauli. "Mimi sielewi kwa nini Mungu anaruhusu mtu kuendelea kuishi wakati mtu huyo angefurahi kuzikwa katika udongo"
# ambao hushangilia mno na kufurahi
Msemo wa "hufurahia sana" kimsingi unamaanisha kitu kimoja kama "furaha." Pamoja, misemo yote miwili inatilia mkazo wa nguvu ya furaha. "mtu ambaye ana furaha sana"
# alionapo kaburi
Hii ni njia ya heshima ya kumaanisha kufa. "wakati yeye akifa na anaweza kuzikwa"
# kaburi
Hapa kaburi linawakilisha kifo.