sw_tn/gal/04/intro.md

24 lines
1.3 KiB
Markdown

# Wagalatia 04 Maelezo ya Jumla
## Muundo na upangiliaji
Baadhi ya tafsiri huweka kila mstari wa mashairi upande wa kulia zaidi kuliko maandiko yote ili iwe rahisi kusoma. ULB inafanya hivi kwa mstari wa 27, ambao umenukuliwa kutoka Agano la Kale.
## Dhana maalum katika sura hii
### Uwana
Uwana ni suala ngumu. Wasomi wana maoni mengi juu ya uwana wa Israeli. Paulo anatumia uwana wa kufundisha jinsi kuwa chini ya sheria hutofautiana na kuwa huru katika Kristo. Si wote wa uzao wa Abrahamu ambao ni wao waliorithi ahadi za Mungu kwake. Uzazi wake tu kupitia Isaka na Yakobo walirithi ahadi. Na Mungu huweka katika familia yake wale tu wanaomfuata Abrahamu kiroho kupitia imani. Wao ni watoto wa Mungu wenye urithi. Paulo anawaita "watoto wa ahadi." (See: [[rc://*/tw/dict/bible/kt/inherit]], [[rc://*/tw/dict/bible/kt/promise]], [[rc://*/tw/dict/bible/kt/spirit]] and [[rc://*/tw/dict/bible/kt/faith]] and [[rc://*/tw/dict/bible/kt/adoption]])
## Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii
### Abba, Baba
"Abba" ni neno la Kiaramu. Katika Israeli ya kale, watu walitumia kwa usawa kutaja baba zao. Paulo "hufasiri" sauti zake kwa kuandika kwa herufi za Kigiriki. (See: [[rc://*/ta/man/translate/translate-transliterate]])
## Links:
* __[Galatians 4:1](../../gal/04/01.md)__
__[<<](../03/intro.md) | [>>](../05/intro.md)__