sw_tn/eph/front/intro.md

6.4 KiB

Utangulizi wa Waefeso

Sehemu ya 1: Utangulizi wa Ujumla

Maelezo ya Kitabu cha Waefeso

  1. Salamu na sala kwa baraka za kiroho katika Kristo (1:1-23)
  2. Dhambi na wokovu (2:1-10)
  3. Umoja pamoja na amani (2:11-22)
  4. Siri ya Kristo ndani yenu, amejulishwa (3:1-13)
  5. Maombi kwa ajili ya utajiri wa utukufu wake ili kuwafanya kuwa na nguvu (3:14-21)
  6. Umoja wa Roho, kujenga Mwili wa Kristo (4: 1-16)
  7. Maisha mapya (4:17-32)
  8. Waigaji wa Mungu (5:1-21)
  9. Wake na waume; watoto na wazazi; watumwa na mabwana (5:22-6:9)
  10. Silaha za Mungu (6:10-20)
  11. Salamu ya mwisho (6:21-24)

Nani aliandika kitabu cha Waefeso?

Paulo aliaandika Waefeso. Paulo alikuwa anatoka mji wa Tarso. Alijulikana pia kama Saulo mwanzoni. Kabla kuwa Mkristo, alikuwa Mfarisayo na kuwatesa Wakristo. Baada ya kuwa Mkristo alitembea mara kadhaa kwa ardhi ya Warumi huku akiambia watu kuhusu Yesu.

Mtume Paulo alisaidia kuanzisha kanisa la Efeso wakati moja wa safari zake. Pia akaishi na Waefeso kwa mwaka moja na nusu akiwasaidia waumini. Pengine Paulo aliandika barua hii angali kwenye jela wa Roma.

Kitabu cha Waefeso ni kuhusu nini?

Paulo aliwaandikia barua hii Wakristo wa Waefeso kuwaeleza upendo wake Mungu kwao kupitia Yesu Kristo. Alieleza baraka Mungu alikuwa anawapa kwa sababu walikuwa wameunganishwa pamoja na Kristo. Aliwaeleza waumini wote kwamba walikuwa umoja na haikujari kama mtu ni Myahudi au Wayunani.

Je, kichwa cha kitabu hiki kinapaswa kutafsiriwaje?

Watafsiri wanaweza kuchagua kuita kitabu hiki kwa kichwa chake cha asili, "Waefeso." Au wanaweza kuchagua kichwa wazi, kama "Barua ya Paulo kwa Kanisa la Efeso" au "Barua kwa Wakristo huko Efeso." (See: rc://*/ta/man/translate/translate-names)

Sehemu ya 2: Dhana muhimu za Kidini na za Kitamaduni

Je, ni nini "ukweli uliofichwa" katika Kitabu cha Waefeso?

Maneno yaliyotafsiriwa katika ULB kama "ukweli uliofichwa" au "uliofichwa" hutokea mara sita. Kwa hiyo Paulo alimaanisha kitu ambacho Mungu alipaswa kuwafunulia wanadamu kwa sababu hawakuweza kukijua wenyewe. Daima ilikuwa inahusu jinsi Mungu alivyopanga kuokoa wanadamu. Wakati mwingine ilikuwa juu ya mpango wake wa kufanya amani kati yake na wanadamu. Wakati mwingine ilikuwa juu ya mpango wake wa kuunganisha Wayahudi na Wayunani kupitia Kristo. Wayunani sasa wanaweza kufaidika na ahadi za Kristo wakiwa sawa na Wayahudi.

Je, Paulo alisema nini juu ya wokovu na kuishi kwa haki?

Paulo alisema mengi juu ya wokovu na kuishi kwa haki katika barua hii na katika barua zake nyingi. Alisema kuwa Mungu amekuwa na wema na kuwaokoa Wakristo kwa sababu wanaamini Yesu. Kwa hiyo, baada ya kuwa Wakristo, wanapaswa kuishi kwa njia ya haki ili kuonyesha kuwa wana imani katika Kristo. (See: rc://*/tw/dict/bible/kt/righteous)

Sehemu ya 3: Masuala muhimu ya Tafsiri

"Wewe" kutumika kwa umoja na wingi

Katika kitabu hiki, neno "Mimi" linamaanisha Paulo. Neno "nyinyi" ni karibu kila mara na linawakilisha waumini ambao wanaweza kusoma barua hii, isipokuwa: 5:14, 6:2, na 6:3. (See: rc://*/ta/man/translate/figs-you)

Je, Paulo alimaanisha nini na "Upekee

Wakati Paulo alizungumza kuhusu "nafsi mpya" au "mtu mpya," alimaanisha hali mpya ambayo muumini anapokea kutoka kwa Roho Mtakatifu. Hali hii mpya iliumbwa kwa mfano wa Mungu (Angalia: 4:24). Maneno "mtu mpya" hutumiwa pia kwa ajili ya Mungu kuleta amani kati ya Wayahudi na Wayunani. Mungu aliwaunganisha kama watu mmoja ambao ni wake (Tazama: 2:15).

Paulo alimaanisha nini na "nafsi mpya" au "mtu mpya"?

Wakati Paulo alizungumza kuhusu "nafsi mpya" au "mtu mpya," alimaanisha hali mpya ambayo muumini anapokea kutoka kwa Roho Mtakatifu. Hali hii mpya iliumbwa kwa mfano wa Mungu (Angalia: 4:24). Maneno "mtu mpya" hutumiwa pia kwa ajili ya Mungu kuleta amani kati ya Wayahudi na Wayunani. Mungu aliwaunganisha kama watu mmoja ambao ni wake (Tazama: 2:15)

Je, mawazo ya "takatifu" na "takasa" yanawakilishwa vipi katika Waefeso katika ULB?

Maandiko hutumia maneno kama hayo ili kuonyesha yoyote kati ya mawazo mbalimbali. Kwa sababu hii, mara nyingi ni vigumu kwa watafsiri kuyawakilisha vizuri katika tafsiri zao. Katika kutafsiri kwa Kiingereza, ULB inatumia kanuni zifuatazo:

Wakati mwingine maana katika kifungu ina maana ya utakatifu wa maadili. Hasa muhimu kwa kuelewa injili ni matumizi ya "takatifu" kuonyesha ukweli kwamba Mungu anawaona Wakristo kama wasio na dhambi kwa sababu wameungana na Yesu Kristo. Matumizi mengine ya "takatifu" ni kueleza wazo kwamba Mungu ni mkamilifu na hana hatia. Matumizi ya tatu ni kueleza wazo kwamba Wakristo wanapaswa kuwa na mwenendo isiyo na hatia, na kasoro katika maisha yao. Katika hali hizi, ULB inatumia "takatifu," "Mungu mtakatifu," "watakatifu," au "watu watakatifu." (Angalia: 1:1, 4)

Wakati mwingine maana katika kifungu inaonyesha Wakristo bila kuashiria jukumu fulani wanalopaswa kufanya. Katika hali hizi, ULB inatumia "mwumini" au "waumini."

Wakati mwingine maana katika kifungu kinaashiria wazo la mtu au kitu kiichowekwa wakfu kwa Mungu pekee. Katika hali hizi, ULB inatumia "kutenga," "kukusudia," au "kuhifadhiwa kwa." (Angalia: 3:5)

UDB mara nyingi husaidia wakati watafsiri wanafikiri juu ya jinsi ya kuwakilisha mawazo haya katika tafsiri zao wenyewe.

Je, Paulo alimaanisha nini kwa maneno "katika Kristo," "katika Bwana," nk?

Aina hii ya usemi hutokea katika 1:1, 3, 4, 6, 7, 9, 10, 11, 12, 13, 15, 20; 2:6, 7, 10, 13, 15, 16, 18, 21, 22; 3:5, 6, 9, 11, 12, 21; 4:1, 17, 21, 32; 5:8, 18, 19; 6:1, 10, 18, 21. Paulo alimaanisha kueleza wazo la muungano wa karibu sana kati ya Kristo na waumini. Tafadhali angalia utangulizi wa Kitabu cha Warumi kwa maelezo zaidi juu ya aina hii ya usemi.

Je, ni masuala gani muhimu katika Kitabu cha Waefeso?

  • "katika Efeso" (1:1). Kadhaa ya maandiko ya awali hayajajumuisha maneno haya, lakini labda yamo katika barua ya awali. ULB, UDB, na tafsiri nyingi za kisasa zinayajumuisha.
  • "kwa sababu sisi ni viungo vya mwili wake" (5:30). Tafsiri nyingi za kisasa, ikiwa ni pamoja na ULB na UDB, husoma kwa njia hii. Baadhi ya matoleo ya zamani yanasoma, "kwa sababu sisi ni viungo vya mwili wake na mifupa yake." Watafsiri wanaweza kuamua kuchagua usomaji wa pili ikiwa matoleo mengine katika eneo lao yanafanana hivyo. Ikiwa watafsiri wanachagua usomaji wa pili, wanapaswa kuweka maneno ya ziada ndani ya mabano ya mraba ([]) ili kuonyesha kwamba labda asili yao sio Kitabu cha Waefeso.

(See: rc://*/ta/man/translate/translate-textvariants)