sw_tn/psa/051/007.md

32 lines
1.4 KiB
Markdown

# Nitakase ... nitakuwa msafi ... nioshe ... nitakuwa mweupe zaidi ya theluji
Kukubalika kwa Mungu kunazungumziwa kama kuwa msafi au mweupe. Mungu huwafanya watu kukubalika kwa kusamehe dhambi zao.
# Nitakase kwa hisopo
Mwandishi anamzungumzia Mungu kana kwamba Mungu ni kuhani ambaye humwaga maji juu yake kumfanya akubalike kwa Mungu. "Nifanye nikubalike kwa kunimwagia maji na hisopo" au "Nisamehe kwa dhambi zangu ili nikubalike kwako"
# hisopo
Huu ni mmea ambao kuhani alitumia kunyunyizia maji au damu juu ya watu au vitu kuvifanya visafi kiutaratibu, yaani, kukubalika kwa Mungu.
# mweupe zaidi ya theluji
Kutokuwa na dhambi kunazungumziwa kama kuwa mweupe. "mweupe sana"
# furaha na shangwe
Maneno haya mawili yana maana moja na yana sisitiza hamu yake kusikia mambo ya furaha.
# ili kwamba mifupa uliyovunja ifurahi
Kujisikia huzuni kali inazungumziwa kana kwamba mifupa yake imevunjika. "Kwa kuwa umesababisha huzuni kali ndani yangu. Acha nifurahi tena!"
# Ficha uso wako mbali na dhambi zangu
Kufikiria kuhusu dhambi za mtu inazungumziwa kama kuziona. Kusamehe au kukataa kuwaza kuhusu dhambi inazungumziwa kama kuchagua kutoziona. "Usizitazame dhambi zangu" au "Usikumbuke dhambi zangu"
# wekea doa udhalimu wangu
Kusamehe au kukataa kuwaza kuhusu dhambi inazungumziwa kama kati ya 1) kuziwekea doa au 2) kufuta kumbukumbu iliyoandikwa ya dhambi. "samehe dhambi zangu kama mtu anafuta kitu" au "samehe dhambi zangu kama mtu anayefuta kumbukumbu ya dhambi"