sw_tn/psa/051/001.md

48 lines
1.5 KiB
Markdown

# Taarifa ya Jumla:
Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.
# Taarifa ya Jumla:
Katika zaburi hii Daudi anamwomba Mungu msamaha.
# Kwa mwanamuziki mkuu
"Hii ni kwa kiongozi wa muziki kutumia katika kuabudu"
# Zaburi ya Daudi
Maana zinazowezekana ni 1) Daudi aliiandika zaburi au 2) zaburi inamhusu Daudi au 3) zaburi iko katika mtindo wa zaburi za Daudi.
# wakati nabii Nathani alipokuja kwake
Inaweza kuelezwa wazi Nathani alifanya nini alipokuja kwa Daudi, kwa sababu zaburi hii ni majibu ya hayo. "wakati nabii Nathani alipokuja kwa Daudi na kumkemea"
# alipolala na Bathsheba
"baada ya Daudi kulala na Bathsheba"
# kwa ajili ya umati wa matendo yako ya huruma
"kwa sababu unafanya mambo mengi sana ya huruma"
# weka doa makosa yangu
Kusamehe dhambi inazungumziwa kana kwamba ni kati ya 1) kuwekea doa au 2) kufuta kumbukumbu za dhambi. "samehe dhambi zanguu kama mtu anazifuta" au "sahau dhambi zangu kama mtu anayefuta kumbukumbu za dhambi"
# Nioshe kikamili kutokana na udhalimu wangu ... nisafishe na dhambi zangu
Misemo hii miwili inamaanisha kitu kimoja.
# Nioshe kikamili kutokana na udhalimu wangu
Kukubaliwa na Mungu kunazungumziwa kama kuwa msafi. Mungu huwafanya watu kukubalika kwa kusamehe dhambi zao. "Osha dhambi zangu zote" au "Samehe dhambi zangu zote ili nikubalike kwako"
# kikamili
"kikamilifu"
# nisafishe na dhambi zangu
Kukubalika kwa Mungu kunazungumziwa kama kuwa msafi. Mungu huwafanya watu kukubalika kwa kusamehe dhambi zao. "Nifanye kuwa msafi na dhambi yangu" au "nisamehe kwa dhambi yangu ili niwe msafi"