sw_tn/rom/16/17.md

956 B

Kauli unganishi

Paulo anatoa onyo la mwisho kwa waumini kuhusu umoja na kuishi kwa ajili ya Mungu

tafakari juu ya

"kuwa waangalifu kwa"

ambao wanasababisha mgawanyiko na vipingamizi

"ambao wanasababisha waumini kubishana kila mmoja kwa mwingine na kuacha kuwa na imani kwa Mungu"

Wanakwenda kinyume na mafundisho ambayo mmekwisha kujifunza

'Wanafundisha mafundisho ambayo hayakubaliani na ukweli mliokwisha jifunza tayari"

Geukeni mtoke kwao

"jitengeni mbali na wao"

bali kwa matumbo yao wenyewe

Hapa "tumbo" linafafanua tamaa za kimwili. "Lakini wanataka kufurahisha tamaa zao mbaya"

Kwa maneno yao laini na pongezi za uongo

Maneno "laini" na "pongezi za uongo" kimsingi yana maana moja. Paulo anafafanua jinzi gani hawa watu wanavyowadanganya waumini. "kwa kusema mambo ambayo yanaonyesha ni mema na ya kweli"

kutokuwa na hatia

"ambao hawana hatia wanawatumainia wao" au "ambao hawawajui hawa waalimu wanaowatia upumbavu"