forked from WA-Catalog/sw_tn
662 B
662 B
Sentensi unganishi:
Paulo anadhihirisha hasira kuu ya Mungu dhidi ya wanaotenda dhambi.
Kwa kuwa ghadhabu yake
Paulo anaelezea kwa nini watu wanatakiwa kuisikia injili.
Ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa
"Mungu amedhihirisha hasira yake"
Dhidi
"juu ya"
uasi wote na udhalimu wa watu
"uasi wote na mambo ya udhalimu ambayo watu wanayatenda"
kuuficha ukweli
"walificha taarifa za kweli kuhusu Mungu"
ambayo inajulikana kuhusu Mungu inaonekana kwao
"wanaweza kujua kuhusu Mungu kwa sababu ya wanayoyaona"
Kwa kuwa Mungu
Paulo anawaonyesha kwa nini watu wanajua mambo kuhusu Mungu.
Mungu amewaangazia
"Mungu ameyaonyesha hayo kwao"