sw_tn/psa/038/001.md

21 lines
690 B
Markdown

# Taarifa ya Jumla:
Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.
# Zaburi ya Daudi
Maana zinazowezekana ni 1) Daudi aliiandika zaburi au 2) zaburi inamhusu Daudi au 3) zaburi iko katika mtindo wa zaburi za Daudi.
# usinikemee katika hasira yako ... usiniadhibu katika gadhabu yako
Misemo hii inamaana moja na wazo linarudiwa kwa ajili ya mkazo.
# mishale yako inanichoma
Ukali wa adhabu ya Yahwe kwa mwandishi unazungumziwa kana kwamba Yahwe amepiga mishale kwa mwandishi. "Adhabu yako ina maumivu kana kwamba umepiga mishale kwangu"
# mkono wako unanikandamiza chini
Adhabu ya Yahwe kwa mwandishi inazungumziwa kana kwamba Yahwe alikuwa akimponda mwandishi kwa mkono wake.