forked from WA-Catalog/sw_tn
668 B
668 B
Maelezo ya jumla
Nahumu anaongea kwa watu wa Ninawi kana kwamba wao ndiyo mji wenyewe.
Ngome
Neno hili, ambalo lingeweza kutafsiriwa kama " ngome ya jeshi" inarejea milki yote ya Ninawi na Ashuru.
Ngome zako zote zitakuwa kama mitini yenye tini zilizoiva mapema: kama zikitikiswa, zitaangukia kwenye kimywa cha mlaji
Mji wa Ninawi utachukuliwa kwa urahisi kama tunda kutoka kwenye mti.
watu miongoni mwenu ni wanawake
"watu wako ni dhaifu na hawawezi kujilinda wao wenyewe"
bawaba zake
Mihimili mikubwa ya mbao ambayo ilishikilia mageti na haikuwezekana kufungua ukiwa nje ya mji. Kuchomwa moto kwa mihimili kulifanya isiwezekane kufunga mji tena.