forked from WA-Catalog/sw_tn
753 B
753 B
Taarifa ya kijumla:
Yesu anaongea moja kwa moja na Simoni.
Simon, Simon
Yesu alilisema jina lake mara mbili kuonyesha kwamba kile ambacho alikuwa akiseme kwake kilikuwa cha muhimu sana.
awapate, ili awapepete
Neno "awa" linaonyesha mitume wote.
awapepete kama ngano
Hii inamaanisha kwamba Shetani alitaka kuwajaribu mitume ili kupata makosa.
Lakini nimekuombea
Hapa inamaanisha amemuombea kipekee kabisa SImoni.
kwamba imani yako isishindwe
"kwamba utaendelea kuwa na imani" au "utaendelea kunitegemea mimi"
Baada ya kuwa umerudi tena
"Baada ya kuanza kunifuata tena" au "Baada ya kuanza kunitumikia mimi tena"
ndugu zako
Hii inamaanisha wanafunzi wengine wa Yesu. Tafsiri mbadala: "Waamini wenzako" au "mitume wengine."