sw_tn/lev/01/12.md

785 B

Taarifa kwa ujumla

Yahweh anaendelea kumwambia Musa liwapasalo watu kutenda

Naye ataikata...iliyofanywa Kwake kwa moto.

Ajili ya 1:12-13, tazama 1:7 ili uone wingi wa maneno haya yalivyofasiriwa

Naye ataikata

Hapa neno "naye" humaanisha mtu anayetoa dhabihu. Laweza kufasiriwa katika nafsi ya pili. :"Nawe utaikata"

italeta harufu ya kupendeza kwa Yahweh

Yahweh akiwa amependezwa na utoaji dhabihu wa dhati wa aabuduye unamezungumziwa kana kwamba Yahweh alikuwa amependezwa na harufu nzuri ya dhabihu.

itakuwa sadaka ya iliyofanywa...kwa moto.

Yahweh anamwambia Musa kwamba ni lazima makuhani wazichome sadaka zao kwa moto. Sentensi hii inaweza kufasiriwa kwenye muundo tendaji. :"itakuwa sadaka ya kuteketezwa kwangu" au "itakuwa sadaka ya kuteketezwa kwa Yahweh"