sw_tn/deu/31/17.md

33 lines
947 B
Markdown

# Taarifa ya Jumla:
Yahwe anaendelea kuzungumza na Musa.
# hasira yangu itawaka dhidi yao
Yahwe analinganisha hasira na mtu anayewasha moto. Hii inasisitiza nguvu ya Mungu kuangamiza chochote kinachomkasirisha. Hii inaweza kuwekwa katika hali ya kutenda. "Nitawasha hasira yangu dhidi yao" au "Nitakuwa na hasira na wao"
# Nitaficha uso wangu kwao
Hii ni lahaja. "Sitawasaidia"
# watamezwa
Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Nitawameza" au "Nitaruhusu maadui zao kuwameza"
# watamezwa
Hii ni sitiari ya "kuangamizwa kabisa".
# Maafa na taabu nyingi zitawakumba
Hii inaelezea maafa na taabu kama yalikuwa binadamu. "Watapatwa na maafa na taabu nyingi"
# Maafa haya hayajaja kwetu ... kati yetu?
Hii inaelezea maafa na taabu kama yalikuwa binadamu. Swali hili la balagha linaweza kutafsiriwa kama kauli. "Maafa haya yananiangamiza .. kati yetu."
# Mungu hayupo kati yetu
"Mungu hatulindi tena" au "Mungu ametuacha peke yetu"