sw_tn/dan/12/07.md

1.0 KiB

mtu yule aliyevaa nguo za kitani

Hii yaweza kuelezwa katika muundo tendaji. " mtu aliyekuwa amevaa nguo za kitani"

mkondo wa mto

Maana zinazoweza kukubalika 1) malaika alikuwa juu ya mto au 2) malaika alikuwa mbali katika ukingo sambamba na mto.

yeye aishiye milele

"Mungu ambaye anaishi milele"

itakuwa kwa wakati, nyakati, na nusu wakati

Ni vizuri kuiacha katika utata kama ilivyoanza. Na kama utachagua sehemu ya kuanzia, miaka mitatu na nusu huenda itaanza pamoja na matukio ya 12:1.

wakati, nyakati, na nusu wakati

"miaka mitatu na nusu: Maneno "nyakati au wakati" kwa ujumla yanapaswa kufahamika kuwa yanarejelea miaka. Mwaka mmoja na miwili na nusu ni sawa na miaka mitatu na nusu.

mambo haya yote yatakuwa yamemalizika

Hii yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "Mambo haya yote yatatokea"

Mambo haya yote

Katika muda ule ambao malaika alikuwa akiongea na Danieli, hakuna hata tukio hata moja lilikuwa limetokea. Hii kwa uhalisia inarejelea matukio katika 12:1, na huenda yalijumuisha matukio yaliyo katika maono kutoka sura ya 11.