forked from WA-Catalog/sw_tn
29 lines
863 B
Markdown
29 lines
863 B
Markdown
# Waliomba wakisema
|
|
|
|
"Ndipo waumini waliomba" Inamaanisha wote waliokuwemo chumba cha juu waliomba, pengine kwa kuongozwa na mtume mmoja.
|
|
|
|
# Wewe, Bwana, wajua mioyo ya watu wote
|
|
|
|
"Bwana, Wewe wajua msukumo wa ndani na mawazo ya kila mmoja"
|
|
|
|
# hivyo funua yupi kati ya hawa wawili ndiye uliye mteua kuchukua nafasi katika huduma hii ya kitume
|
|
|
|
"Kwa sababu hiyo, Mungu, tuoneshe sisi yupi kwenye watu hawa wawili umemteua kujaza nafasi hii wazi katika matume"
|
|
|
|
# Kutokana na Yuda kukosea na kwenda njia yake mwenyewe
|
|
|
|
Nafasi iliachwa wazi sababu Yuda alimsaliti Yesu, aliondoka, na akafa.
|
|
|
|
# Wakawapigia kura
|
|
|
|
Walitumia kura kuamua kati ya Yusufu na Mathiasi
|
|
|
|
# Kura ikamwangukia Mathiasi
|
|
|
|
Kura iliashiria kwamba Mathiasi alikuwa amechaguliwa kuchukua nafasi ya Yuda
|
|
|
|
# Alihesabiwa pamoja na mtume kumi na mmoja
|
|
|
|
"wanafunzi walimchukulia kuwa ni mmoja wa mitume"
|
|
|