sw_tn/3jn/front/intro.md

2.0 KiB

Utangulizi wa 3 Yohana

Sehemu ya 1: Utangulizi wa Ujumla

Maelezo ya Kitabu cha 3 Yohana

  1. Utangulizi (1:1)
  2. Kutia moyo na maelekezo ya kuonyesha ukarimu (1:2-8)
  3. Diotrefe na Demetrio (1:9-12)
  4. Hitimisho (1:13-14)

Nani aliandika Kitabu cha 3 Yohana?

Barua haina jina la mwandishi. Mwandishi alijitambulisha mwenyewe kama "mzee" (1:1). Barua hii pengine ilikuwa imeandikwa na Mtume Yohana alipokaribia kuaga dunia.

Je, kitabu cha 3 Yohana kinahusu nini?

Yohana aliandika barua hii kwa muumini mmoja aitwaye Gayo. Alimwambia Gayo awe na ukarimu kwa waumini wenzake ambao walikuwa wakisafiri kupitia eneo lake.

Je, kichwa cha kitabu hiki kinapaswa kutafsiriwaje?

Watafsiri wanaweza kuchagua kuita kitabu hiki kwa kichwa chake cha jadi, "3 Yohana" au "Yohana wa Tatu." Au wanaweza kuchagua kichwa cha wazi, kama "Barua ya Tatu Kutoka kwa Yohana" au "Barua ya Tatu Aliyoandika Yohana." (See: rc://en/ta/man/translate/translate-names)

Sehemu ya 2: Dhana muhimu za Kidini na za Kitamaduni

Je, ukarimu ni nini?

Ukarimu ulikuwa dhana muhimu katika Mashariki ya Karibu ya kale. Ilikuwa muhimu kuwa na urafiki kwa wageni au watu wasio wa eneo hilo na kutoa msaada kwao ikiwa wangehitaji. Katika 2 Yohana, Yohana aliwakataza Wakristo kutowaonyesha ukarimu walimu wa uongo. Katika Yohana 3, Yohana aliwahimiza Wakristo kuonyesha ukarimu wageni waaminifu.

Sehemu ya 3: Masuala muhimu ya Tafsiri

Je! Mwandishi hutumuia namuna gani uhusiano wa familia katika barua yake?

Mwandishi alitumia maneno "ndugu" na "watoto" kwa namna ambayo inaweza "inaweza kuleta tatizo. Maandiko mara nyingi hutumia neno "ndugu" kutaja Wayahudi. Lakini katika barua hii, Yohana alitumia neno kuelezea Wakristo. Pia, Yohana aliwaita waumini wengine "watoto" wake. Hawa ni waumini aliowafundisha kumtii Kristo.

Yohana pia alitumia neno "Myunani" kwa njia ambayo inaweza inaweza kuleta tatizo. Maandiko mara nyingi hutumia neno "Myunani" kuwataja watu ambao si Wayahudi. Lakini katika barua hii, Yohana alitumia neno kutaja wale ambao hawakuamini Yesu.