sw_tn/2ti/front/intro.md

3.8 KiB

Utangulizi wa 2 Timotheo

Sehemu ya 1 Utangulizi wa jumla

Muhtasari wa Kitabu cha 2 Timotheo

  1. Paulo anamsalimia Timotheo na kumshauri kuvumilia mateso anapomtumkia Mungu (1:1-2:13).
  2. Paulo anampa Timotheo maelekezo ya kibinafsi (2:14-26)
  3. Paulo anamuonya Timotheo kuhusu matukio yajayo na anamshauri jinsi ya kutekeleza kazi yake kwa Mungu (3:1-4:8)
  4. Paulo anatoa matamshi ya kibinafsi

Nani aliandika kitabu cha 2 Timotheo?

Paulo aliandika kitabu cha 2 Timotheo akiwa gerezani Roma. Hapo awali alijulikana kama Saulo. Alitokea mji wa Tarso. Kabla ya kuwa Mkristo alikuwa Mfarisayo na alikuwa akiwatesa sana Wakristo. Baada ya kuwa Mkristo, alisafiri mara nyingi katika himaya nzima ya Warumi akiwahubiria watu kumhusu Yesu.

Hii ni barua ya pili ya Paulo kwa Timotheo. Timotheo alikuwa mwanafunzi wake na rafiki wake wa karibu. Paulo aliandika barua hii akiwa gerezani Roma.Paulo alikuwa karibu kufa.

Kitabu cha 2 Timotheo kinahusu nini?

Paulo alikuwa amemwacha Timotheo katika mji wa Efeso ili awasaidie waumini huko. Paulo aliandika barua hii kushauri Timotheo kuhusu maswala kadhaa. Maswala aliyozungumzia katika barua hii yalikuwa: onyo kuhusu walimu wa uwongo na kuvumilia katika nyakati za matatizo. Barua hii inaonyesha jinsi Paulo alikuwa anamuandaa Timotheo kuwa kiongozi wa makanisa.

Kichwa cha kitabu hiki kitafsiriwe namna gani?

Watafsiri wanaweza amua kukiita kitabu hiki kutumia jina la asili "2Timotheo" ama wanaweza tumia kichwa cha kueleweka zaidi kama "Barua ya Pili ya Paulo kwa Timotheo", ama "Barua ya Pili Kwa Timotheo."(Tazama: rc://en/ta/man/translate/translate-names)

Sehemu ya 2 Dhana muhimu za kidini na kitamaduni

Ni taswira gani ya mwanajeshi katika 2 Timotheo?

Paulo aliposubiri gerezani akiwa anafahamu kuwa angekufa muda si mrefu, alizungumzia mara nyingi kumhusu mwenyewe kama mwanajeshi wa Kristo. Wanajeshi huwajibika kwa amiri yao jinsi Wakristo wajibikao kwa Kristo. Kama "wanajeshi" wa Kristo, waumini wanapaswa kuheshimu amiri zake hata kama kufanya hivyo kutapelekea hao kufa.

Nini maana ya maandiko kuwa pumzi ya Mungu?

Mungu ndiye mwandishi halisi wa maandiko. Aliwaongoza waandishi binadamu. Hii ina maana kwamba kwa namna moja Mungu alisababisha uandishi wa maandiko na watu. Hii ndiyo maana maandiko yanajulikana pia kama neno la Mungu.Hii inamaanisha vitu vingi kuhusu Bibilia. Kwanza ni kwamba Bibilia haina kasoro na inaweza kuaminiwa. Pili, tunaweza kumtegemea Mungu kulinda maandiko kutokana na wale wanaotaka kuyaharibu. Tatu, neno la Mungu linafaa litafsiriwe katika lugha zote za dunia.

Sehemu ya 3: Maswala muhimu ya tafsiri

Umoja na wingi wa "wewe/nyinyi"

Neno "mimi" katika kitabu hiki linaashiria Paulo. "Wewe" inamaanisha Timotheo. Tofauti ya haya ni 4:22 (Tazama: rc://en/ta/man/translate/figs-exclusive and rc://en/ta/man/translate/figs-you)

Paulo alimaanisha nini na maelezo "ndani ya Kristo" na "ndani ya Bwana" na kadhalika?

Paulo alitaka kuelezea wazo la kuwa na ushirika wa karibu sana kati ya muumini na Kristo. Tafadhali tazama utangulizi wa kitabu cha Warumi kwa maelezo zaidi kuhusu kauli hii.

Ni maswala gani kuu ya kimaandishi katika kitabu cha 2 Timotheo?

Katika aya zifuatazo,matoleo ya kisasa yanatofautiana na matoleo ya kale. Toleo la ULB lina masomo ya kisasa na imeweka masomo ya zamani kwenye tiniwayo(maelezo ya chini). Iwapo tafsiri ya Bibilia inapatikana eneo kwa ujumla, watafsiri wanashauriwa kuzingatia matumizi ya masomo yaliyoko katika matoleo hayo. Kama sivyo, watafsiri wanashauriwa kutumia masomo ya kisasa.

  • "Kwa sababu hii niliteuliwa kuwa mhubiri, mtume na mwalimu."(1:11) Matoleo mengine yanasoma, "Kwa sababu hii,niliteuliwa kuwa mhubiri, mtume na mwalimu wa watu wa Mataifa."
  • "Waonye mbele za Mungu" (2:14). Matoleo mengine ya zamani yanasoma, "Waonye mbele za Bwana."

(See: rc://en/ta/man/jit/translate-textvariants)