sw_tn/2ti/03/01.md

1.2 KiB

Sentensi Unganishi.

Paulo anataka Timotheo ajue ya kuwa katika siku za mwisho watu wataikataa kweri na mateso yatakuja, lakini katika hayo anaweza akalitumaini na kulitegemea andiko takatifu la Mungu.

Nyakati za Hatari.

Hizi zitakuwa ni siku, miezi na hata miaka ambayo Wakristo watakuwa katika hatari.

Wenye kujipenda wenyewe.

Matumizi ya neno "wenyekujipenda" inamaanisha upendo wa kiundugu au upendo wakiurafiki au watu wa familia moja, upendo wa asili kati ya marafiki na Jamaa(ndugu zao). Huu sio ya upendo utokao kwa Mungu.

Wenye majivuno.

Mtu yeyote mwenye kujisemea yeye katika hali ya kujisifu.

Wasiokuwa na Moyo wa kupenda.

"Wasiowapenda wa kwao( familia zao)

Wasio suluhishika

"Wasiokubaliana na mtu yeyote" au " wasio penda kusihi kwa amani na mtu yeyote".

Wasingiziaji.

"Washitaki wa uongo"

Wakali(wenye hasira)

"Katili" au " Mkali" au "watakuwa wakifanya mambo ili kuwaumiza wengine".

Wasiopenda Mema.

" Wenye kuchukia Mema"

Wakaidi.

"asiejali"( mtu wa kijiendea)

Majivuno( wenye viburi)

"Wakifikiri kuwa wao ni bora zaidi kuliko"

Siku za mwisho

Hii inamaanisha kuwa "anazungumzia siku za mbeleni baada ya Nyakati za Paulo. "Baadae kabla ya kurudi kwa Yesu"