sw_tn/2ti/01/06.md

1.1 KiB

Maelezo yanayounganisha:

Paulo anamtia moyo Timotheo kuishi kwa nguvu, upendo, nidhamu na kutokuona aibu kwa sababu ya mateso ya Paulo gerezani kwa sababu ya imani ya Paulo kwa Kristo.

Hii ndiyo sababu

"Kwa sababu hii" au "Kwa sababu ya imani yako ya kweli kwa Yesu" au "Kea sababu una imani ya kweli kwa Yesu"

Nakukumbusha

"Nakukumbusha wewe" au "Nakwambia tena wewe"

fufua karama ya Mungu iliyo ndani yako kwa kuwekewa mikono yangu

Paulo alimuwekea Timotheo mikono, kumkabidhi roho mtakatifu na uwezo wa kiroho au zawadi juu yake. Paulo anamwambia "afufue" ule uwezo wa kiroho kwenye kazi zake kwa ajili ya Kristo.

Kwa kuwa Mungu

"Sababu Mungu"

Mungu hakutupa roho ya woga lakini ya nguvu na upendo na nidhamu.

Paulo alipokea roho toka kwa Mungu. Alipoweka mikono yake juu ya Timotheo, roho yule yule alikuja juu ya Timotheo. Roho huyu hakusababisha wamuogope Mungu au watu wengine.

Roho wa ... nidhamu

Inaweza kumaanisha "Roho wa mungu anaweza kuwasaidia kujizuia wenyewe" au 2) "Roho wa Mungu anatusaidia sisi kuwarekebisha wengine wanaofanya makosa."