sw_tn/2ti/01/01.md

1.1 KiB

Paulo

"Toka kwa Paulo" au "Mimi, Paulo, naandika barua hii"

Kwa mapenzi ya Mungu

"kwa sababu ya mapenzi ya Mungu" au "kwa sababu Mungu anataka." Pauli alikuwa mtume kwa sababu Mungu alitakaPaulo awe mtume sio kwa sababu wanadamu walimchagua.

Sawasawa na

Inaweza kuwa na maana 1)"kuweka pamoja na," ikimaanisha kama Mungu alivyoahidi kuwa Yesu uhai, alimfanya Paulo kuwa mtume au 2) "kwa kusudi la,"ikimaanisha kuwaMungu alimteua Paulo kuwaambia wengine kuhusu ahadi ya Mungu ya uhai katika Yesu.

Ahadi ya uhai iliyo ndani ya Yesu Kristo

"Mungu aliahidi kuwafanya wale waliondani ya Kristo Yesu kuwa hai"

Mwana mpendwa

"mwana mpenzi" au "mwana apendwaye" au "mwana ninayempenda." Timotheo aliokolewa na Kristo kwa kupitia Paulo, na hivyo Paulo anamchukulia kama mtoto wake.

Neema, rehema, na amani toka

"Na neema, rehema na amani iwe kwako toka" au " Na upate neema, rehema, na amani toka"

Mungu Baba

"Mungu ambaye ni Baba yetu"

Na Kristo Yesu Bwana wetu

"na Kristo Yesu ambaye ni Bwana wetu"

Maelezo ya jumla.

Kwenye kitabu hiki neno "sisi" inawazungumzia Paulo na Timotheo pamoja na waamini wote.