sw_tn/2pe/front/intro.md

3.2 KiB

Utangulizi wa 2 Petero

Sehemu ya 1: Maelezo kwa jumla

Muhtasari wa kitabu cha 2 Petero

  1. Utangulizi (1:1-2)
  2. Kukumbusha kuishi maisha mema kwa sababu Mungu ametuwezesha (1:3-21)
  3. Onyo kuhusu walimu wa uongo (2:1-22)
  4. Kutia moyo kujiandaa kwa ujio wa pili wa Yesu (3:1-17)

Nani aliandika kitabu cha 2 Petero?

Mwandishi anajitambulisha kama Simoni Petero. Petero alikuwa mtume. Pia aliandika 1 Petero. Kuna uwezekano Petero aliandika barua hii akiwa gerezani Roma muda mfupi kabla ya kifo chake. Petero aliita barua hii kama barua ya pili na kwa sababu hiyo tunaiorodhesha baada ya 1 Petero. Aliandikia barua hii kwa hadhira moja ya barua yake ya kwanza. Kuna uwezekano hadhira hii ilikuwa ni Wakristo waliotawanyika katika inchi za Asia Ndogo.

Kitabu cha 2 Petero kinahusu nini?

Petero aliandika barua hii kuwapa moyo waumini waishi maisha mema. Aliwaonya kuhusu walimu waongo waliosema Yesu alikuwa anachukua muda mrefu kurudi. Aliwaambia Yesu hakuchelewa kurudi ila ni Mungu alikuwa anawapatia watu muda wa kutubu ili waokolewe.

Kichwa cha kitabu hiki kinastahili kutafsiriwa namna gani?

Watafsiri wanaweza kukiita kitabu hiki kutumia jina lake la kitamaduni, "2 Petero" ama "Petero wa Pili" ama wanawezatumia kichwa kinachoeleweka zaidi kama, "Barua ya Pili kutoka kwa Petero" ama "Barua ya pili aliyoandika Petero" (Tazama: rc://en/ta/man/translate/translate-names)

Sehemu ya 2: Dhana muhimu za kidini na kitamaduni

Ni watu gani Petero aliwakemea?

Labda watu Petero aliwakemea ni watu waliojulikana kwa jina la Wagnostiki. Walimu hawa waliharibu mafundisho ya maandiko matakatifu kwa manufaa yao wenyewe. Waliishi maisha maovu na wakafundisha watu kuishi hivyo .

Nini maana ya kwamba Mungu aliongoza maandiko?

Mafundisho ya Maandiko ni muhimu sana. 2 Petero inawasaidia wasomaji kuelewa kwamba ingawa kila mwandishi wa maandiko ana njia yake ya kipekee ya kuandika, Mungu ndiye mwandishi wa kipekee wa maandiko. (1:20-12)

Sehemu ya 3: Maswala muhimu ya tafsiri

Umoja na wingi wa "Wewe" na "Nyinyi"

Katika kitabu hiki, neno "mimi" linaashiria Petero. Pia neno "Nyinyi" linaashiria hadhira ya Petero. (Tazama: rc://en/ta/man/translate/figs-exclusive and rc://en/ta/man/translate/figs-you)

Ni maswala gani muhimu katika maandiko ya kitabu cha 2 Petero?

Katika mistari ifuatayo, matoleo ya kisasa ya Bibilia yanatofautiana na matoleo ya kale. Toleo la ULB lina masomo ya kisasa na linaweka masomo ya zamani kama maelezo ya chini. Kama tafsiri ya Bibilia iko katika eneo kwa ujumla, watafsiri wanapaswa kuzingatia masomo ya matoleo hayo. Kama si hivyo, wanapaswa kufuata masomo ya kisasa.

  • "Kuwekwa katika minyororo ya giza la chini hadi hukumu" (2:4) Matoleo mengine ya kisasa na ya zamani yana, "Kuwekwa katika mashimo ya giza la chini mpaka hukumu".
  • "Wanafurahia matendo ya uongo wakati wakiwa katika karamu na nyinyi" (2:13) Matoleo mengine yana, "Wanafurahia matendo yao wakati wanasherehekea nanyi katika karamu za upendo."
  • "Beori"(2:15) matoleo mengine yanasoma, "Bosori".
  • "Vitu vya asili vitachomwa kwa moto na ardhi na matendo yao yatatambulishwa" (3;10). Matoleo mengine yana, "Vitu vya asili vitachomwa kwa moto na ardhi na matendo yaliyomo vitachomeka."

(See: rc://en/ta/man/jit/translate-textvariants)