1.5 KiB
hakuacha dhambi za Yeroboamu mwana wa Nebati
Hii inamzungumzia Yehu akifanya dhambi zile zile ambazo Yeroboamu alizozifanya, kana kwamba dhambi za Yeroboamu zilikuwa sehemu ambayo Yehu hakuziacha. "hakuacha kufanya aina ya dhambi ambazo Yeroboamu mwana wa Nabeti alizifanya" (UDB)
Nabeti
Hili ni jina la kiume
dhambi ya Israeli
Hapa "Israeli" inarejea kwa watu walioshi huko. "dhambi ya watu wa Israeli"
katika kutimiza
"katika kutekeleza" au "katika kukamlisha"
kile kilicho sahihi katika macho wangu
Macho yanawakilisha kuona, na kuona kunawakilisha mawazo au hukumu. "Kile nilichohukumu kuwa sahihi" au "kile nifikiriacho kuwa sawa"
nyumba ya Ahabu
Hapa "nyumba" ya Ahabu inarejea kwa "familia" yake." "familia ya Ahabu"
yote hayo yalikuwa katika moyo wangu
Hapa "moyo" unawakilisha "tamaa" "yote ninayoyatamani kwa ajili yako kufanya" au "yote ambayo ninayoyataka uyafanye"
kukaa juu ya kiti cha kifalme
"kuwa wafalme"
hata kizazi cha nne
"hata kizazi cha 4" au "kwa vizazi vinne vijavyo." Hii inarejea kwa mwana wake, mjukuu, kitukuu, na nyanya.
Yahwe hakuwa makini kutembea katika sheria ya Yahwe
Hapa "kutembea" inarejea kwa "kuishi." "Yehu hakuwa makini kuishi kulingana na sheria ya Yahwe"
kwa moyo wake wote
Hapa "moyo" inarejea kwa matashi ya mtu na tamaa. "katika kila kitu alichokifanya"
Hakuzigeukia dhambi za Yeroboamu
Ku "geukia" kutoka kwenye kitu inamaanisha kuacha kukifanya. "Yehu hakuacha kufanya dhambi kama alivyofanya Yeroboamu"