sw_tn/2jn/front/intro.md

2.1 KiB

Utangulizi wa 2 Yohana

Sehemu ya 1: Utangulizi wa Ujumla

Maelezo ya Kitabu cha 2 Yohana

  1. Salamu (1:1-3)
  2. Kutia moyo na amri kubwa (1:4-6)
  3. Onyo kuhusu walimu wa uongo (1:7-11)
  4. Salamu kutoka kwa waumini wenzake (1:12-13)

Nani aliandika Kitabu cha 2 Yohana?

Barua haina jina la mwandishi. Mwandishi alijitambulisha mwenyewe kama "mzee." Barua hii pengine ilikuwa imeandikwa na Mtume Yohana alipokaribia kuaga dunia. Maudhui ya 2 Yohana inafanana na yale yaliyo katika Injili ya Yohana.

Je, kitabu cha 2 Yohana kinahusu nini?

Yohana aliandika barua hii kwa mtu aliyemwita "mwanamke aliyechaguliwa" na "watoto wake" (1:1). Hii inaweza kutaja rafiki maalum na watoto wake. Au inaweza kutaja kundi fulani la waumini au waumini kwa ujumla. Kusudi la Yohana la kuandika barua hii lilikuwa kuwaonya wasikilizaji wake kuhusu walimu wa uongo. Yohana hakutaka waumini wawasaidie au watoe fedha kwa walimu wa uongo. (See: rc://en/ta/man/translate/figs-metaphor)

Je, kichwa cha kitabu hiki kinapaswa kutafsiriwaje?

Watafsiri wanaweza kuchagua kuita kitabu hiki kwa kichwa chake cha jadi, "2 Yohana" au "Yohana wa Pili." Au wanaweza kuchagua kichwa cha wazi, kama "Barua ya Pili Kutoka kwa Yohana" au "Barua ya Pili Aliyoandika Yohana." (See: rc://en/ta/man/translate/translate-names)

Sehemu ya 2: Dhana muhimu za Kidini na za Kitamaduni

Je, ukarimu ni nini?

Ukarimu ulikuwa dhana muhimu katika Mashariki ya Karibu ya kale. Ilikuwa muhimu kuwa na urafiki kwa wageni au watu wasio wa eneo hilo na kutoa msaada kwao ikiwa wangehitaji. Yohana alitaka waumini kuonyesha ukarimu kwa wageni. Hata hivyo, hakutaka waumini kuwa wakarimu kwa walimu wa uongo.

Je, ni watu gani ambao Yohana alizungumza dhidi yao?

Watu ambao Yohana alizungumza dhidi yao huenda walikuwa wale ambao watajulikana kama Wagnostiki. Watu hawa waliamini kwamba dunia ilikuwa mbaya. Kwa kuwa waliamini kwamba Yesu alikuwa wa kiungu, walikanusha kwamba alikuwa mwanadamu kweli. Hii ni kwa sababu walidhani kuwa Mungu hangeweza kuwa mwanadamu kwa sababu mwili ni mbaya. (See: rc://en/tw/dict/bible/kt/evil)