sw_tn/2co/08/intro.md

1.4 KiB

2 Wakorintho 08 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

Sura za 8 na 9 zinaanza sehemu mpya. Paulo anaandika kuhusu jinsi makanisa ya Ugiriki yalivyowasaidia waumini maskini huko Yerusalemu.

Baadhi ya tafsiri huweka nukuu kutoka kwenye Agano la Kale kwa upande wa kulia zaidi kuliko maandishi yote. ULB inafanya hivi kwa maneno yaliyotajwa kwenye mstari wa 15.

Dhana maalum katika sura hii

Zawadi kwa kanisa huko Yerusalemu

Kanisa la Korintho lilianza kutayarisha kutoa fedha kwa waumini maskini huko Yerusalemu. Makanisa ya Makedonia pia yalitoa kwa ukarimu. Paulo anatuma Tito na waumini wengine wawili huko Korintho ili kuwahimiza Wakorintho kutoa kwa ukarimu. Paulo na wengine watapeleka fedha huko Yerusalemu. Wanataka watu kujua kuwa inafanyika kwa uaminifu.

Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

Sisi

Inawezekana kwamba Paulo anatumia neno "sisi" kuwakilisha Timotheo na yeye mwenyewe. Inaweza pia kuwajumuisha watu wengine.

Kitendawili

"Kitendawili" ni tamko la kweli ambalo linaonekana kuelezea jambo lisilowezekana. Maneno haya katika mstari wa 2 ni kitendawili: "uwingi wa furaha yao na mwisho wa umaskini wao umezalisha utajiri mkubwa wa ukarimu." Katika mstari wa 3 Paulo anaelezea jinsi umaskini wao ulivyozalisha utajiri. Paulo pia hutumia utajiri na umasikini katika vitendawili vingine. (2 Wakorintho 8:2)

<< | >>