sw_tn/2co/04/01.md

1.4 KiB

Sentensi Unganishi

Paulo anaandika kuwa yeye ni mwaminifu katika huduma yake kwa kumhubiri Kristo, siyo kujisifia yeye mwenyewe. Anaonyesha kifo na maisha ya Yesu kwa jinsi alivyoishi ili kwamba maisha yafanye kazi katika maisha ya wakorintho.

Tuna huduma hii

Hapa neno"sisi" linamwakilisha Paulo na watenda kazi wenzake, lakini sasa kwa Wakorintho kwa vile ambavyo Mungu anatuhudumia na anatuonyesha rehema kwa kutubadilisha sisi tuwe zaidi kama yeye.

na kama ambavyo tumeipokea rehema

Tungo hii inaeleza jinsi Paulo na watumishi wenzake wanayo huduma hii" "Ni zawadi ambayo Mungu ameitoa kwao kwa njia ya rehema yake."

tumekataa njia zote za aibu na zilizofichika.

Hii inamaainisha kwamba Paulo na watumishi wenzake walikatataa kufanya "vitu vinavyo aibisha na vilivyofichwa." Haina maana kwamba walikuwa wamevifanya vitu hivi huko nyuma.

njia zote za aibu na zilizofichika

neno "zilizofichika" hufafanua vitu ambavyo ni vya "kuaibisha"

Hatuishi kwa hila

"ishi kwa udanganyifu"

hatulitumii vibaya neno la Mungu

Tungo hii inatumia mawazo mawili yenye ukanusho kuelezea wazo chanya

tunajionyesha wenyewe kwa dhamiri ya kila mtu

Maana yake kwamba wanatoa ushahidi wakutosha kwa kila mtu anayewasikiliza kuamua ikiwa wako sahihi au hapana.

mbele ya Mungu.

Ina maanisha kwenye uwepo wa Mungu. Ufahamu wa Mungu na uthibitisho wa ukweli wa Paulo umetafsiriwa kama Mungu kuweza kuwaona.