sw_tn/1ti/front/intro.md

3.2 KiB

Utangulizi wa 1 Timotheo

Sehemu ya 1 Utangulizi kwa ujumla

Muhtasari wa kitabu cha 1 Timotheo

  1. Salamu (1:1,2)
  2. Paulo na Timotheo
    • Onyo kuhusu walimu wa uongo (1:3-11)
    • Paulo anashukuru kwa kile Kristo amemfanyia katika utume wake (1:12-17).
    • Anamuomba Timotheo kupigania katika vita hivi vya kiroho (1:18-20).
  3. Sala kwa wote (2:1-8)
  4. Wajibu na majukumu kanisani (2:9-6:2)
  5. Maonyo
    • Onyo la pili kuhusu walimu wa uongo (6:3-5)
    • Pesa (6:6-10).
  6. Maelezo kuhusu mtu wa Mungu (6:11-16)
  7. Maelezo kwa Matajiri (6:17-19)
  8. Maneno yakufunga kwa Timotheo (6:20-21)

Nani aliandika kitabu cha 1 Timotheo?

Paulo alikiandika kitabu cha 1 Timotheo. Hapo awali alijulikana kama Saulo. Alitokea mji wa Tarso. Kabla ya kuwa Mkristo alikuwa Mfarisayo na alikuwa akiwatesa sana Wakristo. Baada ya kuwa Mkristo, alisafiri mara nyingi katika himaya nzima ya Warumi akiwahubiria watu kumhusu Yesu.

Kitabo hiki ni barua ya kwanza ya Paulo kwa Timotheo. Timotheo alikuwa mwanafunzi wake na rafiki wake wa karibu. Kuna uwezekano kama Paulo aliandika barua hii akikaribia kufa.

Kitabu cha 1 Timotheo kinahusu nini?

Paulo alikuwa amemwacha Timotheo katika jiji la Efeso kuwasaidia waumini wa huko. Paulo aliandika barua hii kumshauri Timotheo kuhusu maswala mengi. Kati ya maswala aliyoangazia ni swala la kuabudu katika kanisa, na masherti ya waongozi wa kanisa na maonyo kuhusu walimu wa wongo. Barua hii inaonyesha namuna Paulo alifundisha Timotheo kuwa mwongozi wa makanisa.

Kichwa cha kitabu hiki kitafsiriwe namna gani?

Watafsiri wanaweza amua kukiita kitabu hiki kutumia jina lake la kiasili, "1 Timotheo" ama "Timotheo wa Kwanza" ama wanaezatumia kichwa kinachoeleweka zaidi kama "Barua ya Kwanza kwa Timotheo" (Tazama: rc://en/ta/man/translate/translate-names)

Sehemu ya 2: Dhana muhimu za kidini na kitamaduni

Uanafunzi ni nini?

Uanafunzi ni hali ya kuwafanya watu wawe wanafunzi wa Kristo. Lengo kuu la uanafunzi ni kuwafanya Wakristo kuwa kama Kristo. Barua hii inatoa mwelekeo jinsi kiongozi anatakiwa kumfunza Mkristo ambaye hajakomaa. (Tazama: rc://en/tw/dict/bible/kt/disciple)

Sehemu ya 3: Maswala muhimu ya tafsiri

Wingi na umoja wa "wewe"

Neno "mimi" katika kitabu hiki linaashiria Paulo. "Wewe" inamaanisha Timotheo. Tofauti ya haya ni 6:21 (Tazama: rc://en/ta/man/translate/figs-exclusive and rc://en/ta/man/translate/figs-you)

Paulo alimaanisha nini na maelezo "ndani ya Kristo" na "ndani ya Bwana" na kadhalika?

Paulo alitaka kuelezea wazo la kuwa na ushirika wa karibu sana kati ya muumini na Kristo. Tafadhali tazama utangulizi wa kitabu cha Warumi kwa maelezo zaidi kuhusu kauli hii.

Ni maswala gani kuu ya kimaandishi katika kitabu cha 1 Timotheo?

Katika aya ifuatayo,matoleo ya kisasa yanatofautiana na matoleo ya kale. Toleo la ULB lina masomo ya kisasa na imeweka masomo ya zamani kwenye tiniwayo(maelezo ya chini). Iwapo tafsiri ya Bibilia inapatikana eneo kwa ujumla, watafsiri wanashauriwa kuzingatia matumizi ya masomo yaliyoko katika matoleo hayo. Kama sivyo, watafsiri wanashauriwa kutumia masomo ya kisasa.

  • "Utauwa ndiyo njia ya kupata pesa zaidi" Matoleo mengine ya kale yanasoma, "Utauwa ni njia ya kupata pesa zaidi. Jiepushe na vitu hivyo." (6:5).

(See: rc://en/ta/man/jit/translate-textvariants)