sw_tn/1th/front/intro.md

3.8 KiB

Utangulizi wa Wathesalonike 1

Sehemu 1: Utangulizi wa Jumla

Muhtasari wa kitabu cha Wathesalonike 1

  1. Salamu (1:1)
  2. Sala ya Paulo ya shukrani kwa Wakristo wa Thesalonike (1:2-10).
  3. Huduma wa Paulo Thesalonike (2:1-16).
  4. Paulo anashughulikia ukuaji wao wa kiroho
    • Kama mama (2:7)
    • Kama baba (2:11)
  5. Paulo anamtuma Timotheo kwa Wathesalonike na Timotheo anaripoti kwa Paulo kuhusu huduma huo.
  6. Mshauri yanayotekelezeka
    • Maisha ya kumfurahisha Mungu (4:1-12).
    • Starehe ya waliokufa (4:12-18)
    • Kurudi kwa Kristu ni motisha ya maisha ya umungu (5:1-11)
  7. Baraka za mwisho, shukrani na sala.

Nani aliandika Wathesalonike 1

Paulo aliandika Wathesalonike 1. Hapo awali alijulikana kama Saulo. Alitokea mji wa Tarso. Kabla ya kuwa Mkristo alikuwa Mfarisayo na alikuwa akiwatesa sana Wakristo. Baada ya kuwa Mkristo, alisafiri mara nyingi katika ufalme nzima ya Warumi akiwahubiria watu kumhusu Yesu.

Paulo aliandika barua hii akiwa bado anakaa katika mji wa Korinto. Wasomi wengi wanaamini ya kwamba hii ndiyo ilyokuwa barua ya kwanza ya Paulo miongoni mwa barua alizoziandika nyingi.

Kitabu cha Wathesalonike 1 kinahusu nini?

Paulo aliwaandikia barua hii Waumini katika jiji la Thesalonike. Aliandika barua hii baada ya kulazimishwa na Wayahudi kuondoka jiji hilo. Katika barua hii anasema anachukulia ziara yake jijini humu kama iliyozaa matunda ingawa alilazimishwa kuondoka.

Paulo anajibu kwa habari iliyoletwa na Timoteo kuhusu waumini wa Thesalonike.Waumini wa huko walikuwa wanateswa sana. Paulo aliwahimiza kuendelea kuishi maisha yaliyompendeza Mungu. Pia aliwapa moyo kwa kuwaambia kinachofanyika watu wakufapo kabla ya Kristo kurudi.

Kichwa cha kitabu hiki kitafsiriwe vipi?

Watafsiri wanaweza chagua kichwa cha asili kama "Wathesalonike 1" ama "Wathesalonike wa kwanza". Wanaweza pia kuchagua kichwa cha kueleweka zaidi kama "Barua ya Kwanza ya Paulo kwa Wakristo waThesalonike," ama "Barua ya Kwanza kwa Wakristo wa Thesalonike." Tazama: rc://en/ta/man/translate/translate-names)

Sehemu ya 2: Dhana muhimu za kidini na kitamaduni

Nini maana ya "kuja kwa pili kwa Kristo?"

Paulo ameandika mengi kuhusu ujio wa pili wa Kristo duniani. Kristo atakaporudi atawahukumu watu wote duniani. Atatawala vyumbe vyote na kutakuwa na amani kila mahali.

Nini huwafanyikia wanaokufa kabla ya kurudi kwa Kristo?

Paulo aliweka wazi kwamba wote wanaokufa kabla ya kurudi kwa Kristo watafufuka na kuwa na Yesu.Hawatakuwa wafu milele.Paulo aliandika haya kutia moyo Wathesalonike. Hii ni kwa sababu wengi wao walikuwa na wasiwasi kwamba waliokufa wangeachwa nyuma siku kuu ya kurudi kwa Yesu.

Sehemu ya 3: Maswala muhimu ya tafsiri

Paulo alimaanisha nini na matamshi "ndani ya Kristo" na "ndani ya Bwana?"

Paulo alitaka kuelezea dhana ya Mkristo kuwa karibu na Kristo. Tazama utangulizi katika kitabu cha Warumi kwa maelezo zaidi kuhusu swala hili.

Ni maswala gani muhimu katika maandishi ya kitabu cha Wathesalonike 1?

Katika mistari ifuatayo, matoleo ya kale yanatofoautiana na ya kisasa. Toleo la ULB lina masomo ya kisasa na limeweka ya zamani katika maelezo ya chini. Ikiwa kuna utafsiri wa Bibilia katika eneo jumla, watafsiri wanafaa watumie masomo kwenye tafsiri hizo.Kama siyo hivyo Watafsiri wanaombwa kufuata masomo ya kisasa.

  • "Neema na amani viwe nanyi."Matoleo mengine ya zamani husema, "Neema na amani kutoka kwa Baba Mungu wetu na Bwana wetu Yesu Kristo viwe nanyi."1:1
  • "Badala yake tulikuwa wapole miongoni mwenu kama mama anavyowafariji watoto wake." (2:7).Matoleo mengine ya kisasa na ya zamani yanasoma,"Tulikuwa kama watoto wachanga miongoni mwenu, jinsi mama hufariji watoto wake."
  • "Timotheo ndugu yetu na mfanyikazi mwenzetu wa Mungu" (3:2)Matoleo mengine husema, "Timotheo, ndugu na mtumishi wa Mungu."

(See: rc://en/ta/man/jit/translate-textvariants)