sw_tn/1pe/front/intro.md

2.4 KiB

Utangulizi wa 1 Petero

Sehemu ya 1 Utangulizi wa jumla

Muhtasari wa 1 Petero

  1. Utangulizi (1:1-2)
  2. Shukrani kwa ukombozi wa Mungu kwa waumini (1:3-2:10)
  3. Maisha ya Kikristo (2:11-4:11)
  4. Utiaji wa moyo kuvumila wakati wa mateso (4:12-5:11)
  5. Kufunga (5:12-14)

Nani aliandika kitabu cha 1 Petero?

Kitabu cha 1 Petero kilandikwa na mtume Petero. Aliwaandikia Wakristo Wayahudi waliotawanyika katika Asia Ndogo

kitabu cha 1Petero kinahusu nini?

Petero alibainisha kwamba aliandika barua hii kwa ajili ya "kukutia moyo na kushahidia kwamba hii ndiyo neema ya kweli ya Mungu" (5:12). Aliwahimiza Wakristo kuendelea kumtii Mungu hata wakiwa kwenye mateso. Aliwaambia wafanye hivi kwa sababu Yesu angerudi karibuni.Petero pia alitoa maelezo kuhusu kuheshimu watu walio na mamlaka.

Kichwa cha kitabu hiki kitafsiriwe namna gani?

Watafsiri wanweza kuamua kukiita kitabo hiki na jina lake la kiasili, 1 Petero", ama "Petero wa Kwanza" ama wanaweza kuchagua kichwa kinachoeleweka zaidi kama "Barua ya kwanza kutoka kwa Petero" ama "Barua ya kwanza alioandika Petero."(Tazama: rc://en/ta/man/translate/translate-names)

Sehemu ya 2: Dhana muhimu za kidini na Kitamaduni

Wakristo walitendewa kivipi Roma?

Kuna uwezekano Petero alikuwa Roma akiandika barua hii. Aliupa mji wa Roma jina la mfano ya "Babeli" (5:13). Inaonekana wakati Petero anaandika barua hii, Warumi walikuwa wanawatesa vibaya sana Wakristo.

Sehemu ya 3: Maswala muhimu ya tafsiri

Umoja na wingi wa "wewe" na "nyinyi"

Katika kitabu hiki "Mimi" inaashiria Petero isipokuwa kwa sehemu mbili: 1 Petero:1:6 na 1 Petero 2:6. Neno "nyinyi" limetumika kwa wingi kuashiria hadhira ya Petero. (Tazama: : rc://en/ta/man/translate/figs-you)

Ni maswala gani muhimu katika maandishi ya kitabu cha 1 Petero?

  • "Mlizitakasa roho zenu kwa kutii ukweli.Hii ilikuwa ni kwa sababu ya upendo bila unafiki wa kindugu. Kwa hivyo mpendaneni kabisa kutoka moyoni." (1:22). ULB, UDB na matoleo mengine ya kisasa yanasema hivi. Matoleo mengine ya kale yanasoma, "Mlifanya roho zenu safi kwa utiifu wa ukweli kupitia Roho kwa ajili ya upendo bila unafiki wa kindugu, kwa hivyo mpendaneni bila unafiki kutoka rohoni."

Iwapo tafsiri ya Bibilia ipo katika eneo kwa jumla, watafsiri wanafaa kuzingatia kutumia masomo yanayopatikana katika matoleo hayo. Kama sivyo watafsiri wanashauriwa kufuata masomo ya kisasa.

(See: rc://en/ta/man/jit/translate-textvariants)