sw_tn/1jn/front/intro.md

4.4 KiB

Utangulizi wa 1 Yohana

Sehemu ya 1: Utangulizi wa Ujumla

Maelezo ya Kitabu cha 1 Yohana

  1. Utangulizi (1:1-4)
  2. Kuishi Kikristo (1:5-3:10)
  3. Amri ya kupendana (3:11-5:12)
  4. Hitimisho (5:13-21)

Nani aliandika Kitabu cha 1 Yohana?

Kitabu hiki hakitaji mwandishi. Hata hivyo, tangu wakati wa Kikristo wa kwanza, Wakristo wengi wamefikiri kwamba Mtume Yohana ndiye aliyekuwa mwandishi. Yeye pia aliandika Injili ya Yohana.

Je, kitabu cha 1 Yohana kinahusu nini?

Yohana aliandika barua hii kwa Wakristo wakati ambapo walimu wa uongo walikuwa wakiwasumbua. Yohana aliandika barua hii kwa sababu alitaka kuzuia waumini wasitende dhambi. Alitaka kuwalinda waumini dhidi ya mafundisho ya uongo. Na alitaka kuwahakikishia waumini kwamba walikuwa wameokolewa.

Je, kichwa cha kitabu hiki kinapaswa kutafsiriwaje?

Watafsiri wanaweza kuchagua kuita kitabu hiki kwa kichwa chake cha jadi, "1 Yohana" au "Yohana wa Kwanza." Au wanaweza kuchagua kichwa cha wazi, kama "Barua ya Kwanza Kutoka kwa Yohana" au "Barua ya Kwanza Aliyoandika Yohana." (See: rc://en/ta/man/translate/translate-names)

Sehemu ya 2: Dhana muhimu za Kidini na za Kitamaduni

Ni watu wapi ambao Yohana alizungumza dhidi yao?

Watu ambao Yohana alizungumza dhidi yao inawezekana kwamba walikuwa wale ambao wangejulikana kama Wagnostiki. Watu hawa waliamini kwamba dunia ni uovu. Kwa kuwa waliamini kwamba Yesu alikuwa wa kiungu, walikanusha kwamba alikuwa mwanadamu kweli. Hii ni kwa sababu walidhani Mungu hawezi kuwa mwanadamu kwa sababu mwili ni uovu. (See: rc://en/tw/dict/bible/kt/evil)

Sehemu ya 3: Masuala muhimu ya Tafsiri

Maneno "kubaki" na "kuishi" na "kukaa" yana maana gani katika 1 Yohana?

Yohana mara nyingi alitumia maneno "kubaki," "kuishi," na "kukaa" kama sitiari. Yohana alizungumzia muumini kuwa mwaminifu zaidi kwa Yesu na kumjua Yesu vizuri ikiwa neno la Yesu "lilibaki" ndani ya muumini huyo. Pia, Yohana alizungumzia mtu aliyejiunga kiroho na mtu mwingine kana kwamba mtu "aliyebaki" katika mtu mwingine. Wakristo wanasema "kubaki" katika Kristo na kwa Mungu. Baba anasemekana "kubaki" ndani ya Mwana, na Mwana anasemekana"kubaki" ndani ya Baba. Mwana anasemekana "kubaki" katika waumini. Roho Mtakatifu pia anasemekana "kubaki" ndani ya waumini.

Watafsiri wengi wataona kuwa ni vigumu kuwakilisha mawazo haya katika lugha zao kwa njia hiyo hiyo. Kwa mfano, Yohana alitaka kueleza wazo la Mkristo kuwa pamoja na Mungu kiroho wakati alisema, "Yeye asemaye anakaa katika Mungu" (1 Yohana 2: 6). UDB inasema, "Ikiwa tunasema kuwa sisi tuna umoja na Mungu," lakini watafsiri mara nyingi wanapaswa kutumia maneno mengine ambayo yanawasilisha mawazo haya vizuri.

Katika kifungu hicho, "neno la Mungu linakaa ndani yenu" (1 Yohana 2:13), UDB inaelezea wazo hili kama, "unaendelea kutii kile ambacho Mungu anaamuru." Watafsiri wengi wataona kuwa inawezekana kutumia tafsiri hii kama mwongozo.

Je, ni masuala gani muhimu katika Kitabu cha 1 Yohana?

Yafuatayo ni masuala muhimu zaidi ya maandishi katika 1 Yohana:

  • "Na tunawaandikia mambo haya ili furaha yetu iwe kamili." (1:4) ULB, UDB, na matoleo ya kisasa zaidi husoma hivi. Baadhi ya matoleo ya zamani yana, "Na tunawaandikia mambo haya ili furaha yenu iwe kamili."

  • "Na ninyi nyote mnajua ukweli." (2:20) ULB, UDB, na matoleo ya kisasa zaidi yasoma hivi au ifuatavyo: "Na ninyi nyote mna ujuzi." Baadhi ya matoleo ya zamani yana, "na mnajua vitu vyote."

  • "na hivi ndivyo tulivyo!" (3:1). ULB, UDB, na matoleo ya kisasa zaidi kusoma hivi. Baadhi ya maandishi ya zamani yameacha maneno haya.

  • "na kila roho isiyokubali Yesu haitoki kwa Mungu." (4:3) ULB, UDB, na matoleo ya kisasa zaidi yana somo hili. Baadhi ya maandishi ya kale yanasoma, "na kila roho isiyokubali kwamba Yesu amekuja katika mwili sio ya Mungu."

  • "Kwa maana kuna watatu wanaoshuhudia mbinguni: Baba, Neno, na Roho Mtakatifu, na hawa watatu ni mmoja.Nao kuna watatu ambao wanashuhudia duniani: Roho, maji, na damu; na hawa tatu ni kama moja." (5:7-8). ULB, UDB, na matoleo mengine mengi hayasomi hivi. Watafsiri wanashauriwa kutafsiri hii kama ULB inavyofanya. Hata hivyo, ikiwa katika eneo la watafsiri, kuna matoleo ya zamani ya Biblia ambayo yanajumuisha kifungu hiki, watafsiri wanaweza kukijumuisha. Ikiwa imejumuishwa, inapaswa kuwekwa ndani ya mabano ya mraba ([]) ili kuonyesha kwamba labda haipo katika toleo la awali la 1 Yohana. (See: rc://en/ta/man/translate/translate-textvariants)

(See: rc://en/ta/man/jit/translate-textvariants)