sw_tn/1co/13/08.md

1017 B

Upendo

Kumpenda mtu mwingine ni kumjali na kufanya mambo ambayo yatamletea faida au kumnufaisha. Upendo upo aina mbalimbali 1. Upendo unaotoka kwa Mungu huwa unakusudia kuleta mema kwa wengine, huwa haulengi kujinufaisha kwa mtu mmoja. Mungu mwenyewe ni upendo na chanzo cha upendo.

Nabii, unabii

Nabii ni mtu anayeleta ujumbe kutoka kwa Mungu kwenda kwa watu. Mara nyingi manabii huwaonya watu kutoka katika dhambi ili kumtii Mungu. Unabii ni ujumbe unaotolewa na Nabii

Lugha

Katika Biblia neno Lugha humaanisha, lugha za wanadamu zinazotumiwa na makundi mbalimbali ya watu. Wakati mwingine neno Lugha humaanisha lugha ya kiroho ambayo Roho Mtakatifu huwapa waumini kama moja ya "zawadi au karama za Roho"

kujua, maarifa

kujua ni kuelewa kitu au kufahamu jambo, kutambua. maarifa ni neno linalohusiana na habari ambayo watu wanaifahamu.

Kamili

Katka Biblia neno hili humaanisha kukomaa ua kukua katika maisha ya kiroho. Kufanya kitu kikamilike ni kukifanyia kazi hadi kiwe kizuri bila dosari.