sw_tn/rom/10/14.md

1.1 KiB

Basi watawezaje kumwita yeye wasiye mwamini?

Paulo anatumia swali kusisitiza umuhimu wa kupeleka habari njema za Kristo kwa wale ambao hawajasikia. Neno "wale" urejea kwa wale ambao si wa Mungu. "Wale ambao hawamwamini Mungu hawawezi kumwita yeye"

Na watawezaje kuamini katika yeye ambapo hawajamsikia?

Paulo utumia swali jingine kwa sababu ile ile. "Na hawawezi kuamini katika kama hawajasikia ujumbe wake" au "Na hawawezi kuamini katika yeye kama hawajasikia ujumbe kuhusiana na yeye."

kuamini katika

Hapa ina maanisha kukiri kwamba kile mtu alichosema ni kweli.

Na watawezaje kusikia pasipo mhubiri?

Paulo anatumia swali jingine kwa sababu ile ile. "Na hawawezi ujumbe kama hakuna mtu wa kuwambia"

Na watawezaje kuhubiri, mpaka watumwe?

Paulo anatumia swali jingine kwa sababu ile ile. Neno "wale" urejea kwa wale wa Mungu. "Na hawawezi kuwaambia watu wengine ujumbe mpaka mtu awatume"

Ni mzuri miguu ya wale wanaotangaza habari njema za mambo mazuri

Paulo anatumia "miguu" kuwakilisha wale wanaosafiri na kuleta ujumbe kwa wale amba hawajasikia. "Inafurahisha pindi waleta ujumbe huja na kutuambia habari njema."