sw_tn/rom/08/20.md

985 B

Kwa maana uumbaji ulitiishwa chini ya ubatili

"Kwa maana Mungu alisababisha kile alichokiumba kisiweze kufikia lengo ambalo alilolikusudia"

sio kwa mapenzi yake, bali yake yeye aliyevitiisha

Hapa "uumbaji" umeelezwa kama mtu ambaye anaweza kutamani. "sio kwa sababu kwamba hiki ndicho vitu vilivyoumbwa vilihitaji, bali kwasababu ndicho ambacho Mungu alihitaji"

ni katika tumaini kwamba uumbaji wenyewe utawekwa huru

"Kwasababu Mungu alijua kwamba atauokoa uumbaji."

kutoka utumwa hadi uharibifu

Paulo anavilinganisha vitu vyote katika uumbaji na watumwa na "uharibifu" wao. "kutoka kuoza na kufa"

kwenye uhuru wa utukufu wa wana wa Mungu

"na atawaweka huru atakapowapa heshima watoto wake"

Kwa maana twajua ya kuwa uumbaji nao pia unaugua na kuteseka kwa uchungu pamoja hata sasa

Uumbaji unalinganisha na mwanamke anavyougua wakati wa kuzaa mtoto. "Kwa maana twajua ya kuwa kila kitu ambacho Mungu amekiumba kinataka kuwa huru na huugua kama mwanamke anayezaa"