sw_tn/rom/07/07.md

1.1 KiB

Tutasema nini basi?

Paulo anatambulisha mada mpya.

Isiwe hivyo kamwe

"Ndiyo hiyo si kweli!" Msemo huu unatoa kwa nguvu jibu hasi kwa swali la mtego lililotangulia. Unaweza kuwa na msemo unaofanana na huu katika lugha yako ambao unaweza kuutumia hapa.

Mimi nisingeijua dhambi kamwe, isingelikuwa ni kwa njia ya sheria...Lakini dhambi ilichukua nafasi...ikaleta kila aina ya tamaa

Paulo anaifananisha dhambi sawa na mtu ambaye anaweza kutenda.

dhambi ilichukua nafasi kupitia amri na kuleta kila aina ya tamaa ndani yangu

Wakati sheria ya Mungu inatuambi tusifanye jambo, ni kwa sababu tumeambiwa tusifanye ndio maana tunataka tufanye zaidi. "dhambi ilinikumbusha amri kutokutamani vitu viovu, na hivyo nilitamani vitu hivyo viovu zaidi kuliko mwanzo" au "kwa sababu nilitaka kutenda dhambi, wakati niliposikia ile amri ya kutotamani vitu viovu, nilivitamani"

dhambi

"hamu yangu ya kufanya dhambi"

tamaa

Neno hili linajumuisha kwa pamoja hamu ya kumiliki vitu vya wengine na tamaa mbaya ya zinaa.

pasipo sheria, dhambi imekufa

"kama kusingelikuwa na sheria, kusingelikuwa na uvunjifu wa sheria, hivyo kusingelikuwa na dhambi"