sw_tn/rom/06/intro.md

2.0 KiB

Warumi 06 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

Paulo anaanza sura hii kwa kujibu jinsi mtu anavyoweza kupinga kitu ambacho alifundisha katika Sura ya 5. (See: rc://*/ta/man/translate/figs-hypo)

Dhana maalum katika sura hii

Kinyume na Sheria

Katika sura hii, Paulo anapinga mafundisho ya kwamba Wakristo wanaweza kuishi wanavyotaka baada ya kuokolewa. Wasomi wanaita hii "uasi" au kuwa "kinyume na sheria." Kuhamasisha maisha ya kiungu, Paulo anakumbuka gharama kubwa ambayo Yesu alilipa ili Mkristo aokolewe. (See: [[rc:///tw/dict/bible/kt/save]] and [[rc:///tw/dict/bible/kt/godly]])

Watumishi wa dhambi

Kabla ya kumwamini Yesu, dhambi huwafanya watu kuwa watumwa. Mungu huwaachilia Wakristo kutotumikia dhambi. Wana uwezo wa kuchagua kumtumikia Kristo katika maisha yao. Paulo anaelezea kwamba wakati Wakristo wanachagua kutenda dhambii, wao huchagua kutenda kwa hiari yao. (See: [[rc:///tw/dict/bible/kt/faith]] and [[rc:///tw/dict/bible/kt/sin]])

Matunda

Sura hii inatumia taswira ya matunda. Mfano wa matunda mara nyingi inaashiria imani ya mtu inayozalisha matendo mema katika maisha yao. (See: [[rc:///tw/dict/bible/other/fruit]] and [[rc:///tw/dict/bible/kt/righteous]])

Mifano muhimu ya matamshi katika sura hii

Maswali ya uhuishaji

Paulo anatumia maswali ya uhuishaji katika sura hii. Inaonekana nia ya maswali haya ya uhuishaji ni kumfanya msomaji kuona dhambi zake ili amtegemee Yesu. (See: [[rc:///ta/man/translate/figs-rquestion]] and [[rc:///tw/dict/bible/kt/guilt]] and rc://*/tw/dict/bible/kt/sin)

Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

Kifo

Paulo anatumia "kifo" kwa njia nyingi tofauti katika sura hii: kifo cha kimwili, kifo cha kiroho, dhambi inayotawala ndani ya moyo wa mwanadamu, na kumaliza kitu. Anatofautisha dhambi na kifo na maisha mapya yanayotolewa na Kristo na njia mpya Wakristo wanapaswa kuishi baada ya kuokolewa. (See: rc://*/tw/dict/bible/other/death)

<< | >>